Mashabiki wa Simba wamemshukia Mwenyekiti wao wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe.
Mashabiki hao kupitia mitandao mbalimbali wakionyesha wazi kupinga kauli yake dhidi ya beki Shomari Kapombe.
Kapombe ni majeruhi lakini Hans Poppe alionyesha kushangazwa na Kapombe kutorejea uwanjani huku akisisitiza amepona.
Hans Poppe alikwenda mbali zaidi na kutishia akisema arejee acheze au aende kwa kuwa hawawezi kuendelea kumlipa mtu mshahara akiwa nje.
Mashabiki hao wamemtaka Hans Poppe kuwa muungwana hasa baada ya Kapombe kujibu akisema bado ni majeruhi na hawazi kucheza,.
Kapombe amesisitiza kama Simba wako tayari kuvunja mkataba hana tatizo.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App Yetu
Android ===> Bofya hapa
Mashabiki wengine wamemshambulia Hans Poppe kwa lugha chafu wakidai si kauli ya kiongozi anayeweza kuzungumza hivyo badala ya kuzungumza na mchezaji au kuchukua hatua.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini