Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Serikali yalipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

Serikali imelipongeza shirika la utangazaji la Tanzania(TBC) kwa kuendelea kurusha matangazo mubashara katika ziara  mbalimbali za viongozi hapa nchini ikiwemo ziara ya Rais wa Jamhuri Misri hapa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan muda mfupi mara baada ya kuagana na Rais wa Misri katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.

Amesema kuwa shirika hilo la utangazaji linafanya vizuri ambapo limekuwa likihakikisha kuwa kila tukio kubwa limekuwa likirushwa mubashara hivyo kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa wakati muafaka.

“Niwapongeze sana TBC, kwani tangu jana tumekuwa pamoja kwenye mapokezi mpaka leo hii tena wakati wa kumuaga, hivyo hongereni sana na nampongeza mkurugenzi wa TBC kwa kazi nzuri anayoifanya,”amesema Samia Suluhu.

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limekuwa likihakikisha linarusha matangazo mubashara ili kuweza kuifikia jamii moja kwa moja, hivyo kufikisha ujumbe kwa muda muafaka

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017