Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Hii Hapa Orodha Kamili Ya Waliotwaa Tuzo Za Ligi Kuu Na Kikosi Bora Cha Mwaka

Sherehe za Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania zimefanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Mlimani City, huku tuzo 15 zikitolewa kwa wachezaji, viongozi wa mpira mguu nchini.
Ikiwa tofauti na msimu uliopita, msimu huu umeshuhudia vipengele vya tuzo vikiongezeka na kufanya kuwepo kwa tuzo nyingi zaidi.
Waliopata tuzo ni;
Bingwa wa Ligi Kuu – Yanga ( milioni 84)
Mshindi wa pili – Simba (milioni 42)
Mshindi wa tatu – Kagera Sugar (milioni 30)
Mshindi wa nne – Azam FC (milioni 24)
Timu yenye Nidhamu – Mwadui FC (milioni 17.5)
Mwamuzi Bora – Hery Sasii
Mlinda mlango bora – Aishi Salum
Mchezaji anayechipukia – Mbaraka Yusuph
Mchezaji wa kigeni – Haruna Niyozima
Goli bora la msimu – Shiza Kichuya
Mfungaji bora – 14 Saimon Msuva (Yanga), 14 Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting)
Tuzo ya Ismail Khalfan U20 – Shaban Idd Chilunda (Azam FC)
Tuzo ya heshima – Sunday Manara (mchezaji wa zamani Yanga na Taifa Stars)
Kocha Bora – Mecky Maxime


Mchezaji bora – Mohamed Hussein Zimbwe Jnr
KIKOSI BORA CHA MWAKA
Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji mchanganyiko, wachezaji wanaotoka nje na ndani ya nchi wanaocheza Ligi hiyo huku ukitazamwa zaidi mchango wa mchezaji katika timu yak na muda alioutumikia katika msimu.

Waliochanguliwa kuunda kikosi hicho ni :
Aishi Manula (Azam) -Salum Kimenya (Prisons), Mohamed Hussein (Simba) Yahya Mohamed (Azam), Method Mwanjale (Simba) -Kenny Ally (Mbeya City), Saimon Msuva (Yanga), Haruna Niyonzima (Yanga), Shiza Kichuya (Simba)- Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar)na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting)

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017