Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Haji Manara ataja Kilichomchukiza wakati Yanga ikiwatoa Ihefu FA cup

Moja kati ya Maafisa habari ambao wamekuwa na Mbwembwe hasa wanapopata nafasi ya Kuandika au Kuongea kuhusu Mpira Haji Manara wa Simba amekuwa Kivutio sana hasa anapoongelea Utani kwa Yanga na Kuisifia Klabu yake ya Simba.
Baada ya Mchezo kati ya Ihefu na Yanga ulioisha kwa Yanga kupata Ushindi kwa Penati 4 kwa 3 dhidi ya Ihefu ya Mbarali mkoani Mbeya Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram alionekana kuchukizwa na Maamuzi ya Refa wa mchezo huo.
Hata Nyani hutamani pilau,mbeleko za baadhi ya maamuzi ni kichefuchefu..ndio maana baadhi ya team zikienda kwenye international competitions wanatutia aibu tu…Ndegelec!!
Refa huyo msomaji wa kwataunit alitoa tuta dakika za Mwisho kabisa mara baada ya Obrey Chirwa kuangushwa kwenye eneo hatari akielekea Kufunga, Penati ambayo iliwekwa kambani na Obrey Chirwa.

Ile Ishu Ya Simba Kuandika Barua Wakitaka Mechi Yao Na Azam Isogezwe Iko Hivi...





Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ni kama imeanza kuingia mchecheto baada ya kuitaka Bodi ya Ligi (TPLB) kusogeza mbele mechi yake dhidi ya Azam iliyopangwa kuchezwe Februari 11 mwaka huu.

Simba yenye pointi 35, inachuana vikali na Azam wenye 30 katika msimamo wa ligi na Mabingwa watetezi Yanga waliovuna 28, katika kuliwania taji hilo la ubingwa la ligi.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Haji Manara alisema ratiba yao inawapa ugumu kutokana na akili na nguvu zao kuzielekeza kwenye michuano ya kimataifa na Simba imepangwa kucheza Gendarmerie Nationale ya Djibouti kati ya Februari 9-11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Manara alisema, ratiba hiyo inawapa ugumu kwani Simba itacheza na Ruvu Shooting Februari 4 na kucheza na Azam kabla ya kwenda Shinyanga kucheza na Mwadui huku wakiusubiria mchezo wao wa kimataifa.
“Mipango ya Simba ni kufika mbali katika michuano ya Afrika na hiyo ndiyo sababu ya sisi kumchukua kocha Mfaransa, Lechantre (Pierre) ambaye amewahi kuipa ubingwa wa Afcon, Cameroon mwaka 2000.

“Hivyo, basi kama uongozi tumeiomba Bodi ya Ligi kusogeza mbele mchezo wetu dhidi ya Azam ili kutupa nafasi ya kujiandaa na mechi yetu ya kimataifa dhidi ya Wadjibout kwa kuwa tunaona ratiba inabana sana.

“Tupo katika hatua ya mwisho kwa ajili ya kuiandikia bodi ya ligi ili kuwafahamisha mchezo huo usogezwe mbele na kikubwa tunataka kuona Simba ikifanya vema katia michuano hii ya mikubwa Afrika, tunaamini busura itatumika,”alisema Manara.

Kocha Mpya Simba Alia Na Niyonzima , Atoa Kauli Hii…

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Pierre Lechantre amesema anahiyanakumuona kiungo wa kimataifa wa Rwanda Harun Niyonzima akirejea dimbani baada ya kupona majeraha ili kuongeza ushindani katika timu.
Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema kuwa anamfahamu vyema Niyonzim kuwa ni mchezaji mwenye kipaji lakini anahitaji kukiona uwanjani  ili aweze kumpatia nafasi katika kikosi chake.
“Uongozi na benchi la ufundi la timu ya Simba wamenieleza kuhusu Niyonzi na mimi nakubaliana na walisemalo lakini nahitaji kumkumuona uwanjani akithibitisha yasemwayo. Alisema Lechantre.
Niyonzima amekuwa nje ya uwanja  kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi kitu kinachopelea kuhitaji mazoezi binafsi au mwalimu wa kumnoa kuhakikisha anarejea katika kiwango chake cha awali.

Jikumbushe Wafungaji Bora Wa Ligi Kuu Bara Hadi Baada Ya Mechi 15 Kwa Kila Timu

2017/18
Okwi Simba 12
Habib Haji Mbao 7
Mohammed Rashid Prisons 7
Obrey Chirwa Yanga 7
John Bocco Simba 7
Kichuya Simba 6
Ajibu Yanga 5
Marcel Boniventure Majimaji 5
Asante Kwasi Simba 5 Akiwa Lipuli alifunga manne
Paul Nonga Mwadui 4
Eliud Ambokile Mbeya 4
Mbaraka Yusuph Azam 3
Venus Ludovick Kagera 3
Danny Usengimana Singida 3
Eliuter Mpepo Prisons 3
William Lucian  Ndanda 3
Emmanuel Mviyakure Mbao 3
Hamis Mcha Ruvu 3
Paul Peter Azam 2
Edward Christopher Kagera 2
Laudit Mavugo Simba 2
Mohammed Samatta Mbeya 2
Evarist Maganga Mwadui 2
Abdallah Seseme Mwadui 2
Donald Ngoma Yanga 2
Michael Katsaivro Singida 2
Stamili Mbonde Mtibwa 2
Mzamiru Yassin Simba 2
Jafar Kibaya Kagera 2
Emmanuel Martin Yanga 2
Kelvin Sabato Mtibwa 2
Hassan Dilunga Mtibwa 2
Pius Buswita Yanga 2
Yahaya Zayd Azam 2
Peter Mapunda  Majimaji 2
Omary Mponda Ndanda 2
Salim Hamis Mwadui 2
Claide Wigenge Njombe 2

Elinyesia Sumbi Singida 2

Suala La Kujiamini Ubingwa Mapema, Kocha Simba Awapa Neno La Tahadhari Wanasimba





Kutokana na mwendo wa kikosi cha Simba katika Ligi Kuu Bara, wengi wanaamini lazima kitabeba ubingwa.

Kocha Msaidizi wa Simba Mrundi, Masoud Djuma ametamka kuwa ni ngumu kutabiri Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kutua Msimbazi katika mzunguko huu wa pili licha ya kuongoza katika msimamo.

Simba hivi sasa inaongoza katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 35 wakifuatiwa na Azam FC wenye 30 huku Yanga wakishika nafasi ya tatu wakivuna 28.

Djuma alisema bado bingwa wa ligi hajaulikana hivi sasa wakielekea kwenye mzunguko wa pili kutokana na kupishana pointi chache dhidi ya wapinzani wao Yanga na Azam.

Djuma alisema, bado wana kibarua kigumu cha kuhakiisha wanashinda kila mchezo utakaokuwepo mbele yao ili waache kwa idadi kubwa ya pointi wapinzani wao.

“Ili tujihakikishie ubingwa wa ligi kuu, basi tunatakiwa kushinda kila mchezo utakaokuwepo mbele yetu bila ya kuidharau hii timu ndogo au kubwa.

“Hilo tumeshwaambia na tunaendelea kuwakumbusha wachezaji wetu katika vikao tunavyovifanya kila siku kabla ya na baada ya mazoezi kwa kuwasisitiza tupambane ili tujiwekee mazingira mazuri ya ubingwa.


“Kama unavyofahamu tumebakisha kombe moja pekee la ligi kuu, kwani tayari tumelipoteza Kombe la FA, hivyo ili tuuchukue Ubingwa wa ligi ni lazima wachezaji wapambane ndani ya uwanja kwa kupata matokeo mazuri ili tuzidi kuwaacha mbali wapinzani wetu Yanga na Azam waliokuwepo chini yetu,”alisema Djuma.

Kibaka Amuingiza Mjini Pluijm Wamuibia Mkoba wa Fedha

Kibaka Amuingiza Mjini Pluijm Wamuibia Mkoba wa Fedha

MUDA mchache baada ya kushuhudia timu yake ikipata bao la pekee katika dakika za nyongeza dhidi ya Tanzania Prisons juzi, Kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm, alijikuta akiingizwa mjini na vibaka kwa kuibiwa mkoba wa fedha wakati akishangilia bao hilo.

Pluijim aliibiwa mkoba huo uliokuwa na simu aina ya Sumsung Pro 9 yenye thamani ya Sh. 1,575,700,  pochi ('wallet'), leseni ya udereva kwa nchi mbili Tanzania na Ghana, fedha za Dola 100 za Marekani, fedha taslimu Sh. 200,000 za Tanzania na funguo za gari lake aina ya Prado.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Isaya Mbughi, alisema baada ya ushindi huo, mashabiki walishangilia sana kiasi cha mhalifu kutumia mwanya huo kuiba mkoba wa kocha huyo hivyo kulazimika kuripoti polisi na msako mkali kuanza.

Askari wakiongozwa na taarifa za kitengo cha makosa ya mtandao kwa kutumia namba ya simu ya Pluijim iliyokuwamo kwenye mkoba, walifanikiwa kupata begi hilo likiwa limetupwa eneo la mtaa wa Kindai baada ya mwizi kubaini anafuatiliwa na polisi. 

Mbughi alisema kweye mkoba huo polisi walifanikiwa kukuta vitu vyote isipokuwa fedha ambazo mwizi alitoweka nazo.

Pluijim alipatiwa vitu vyake vyote isipokuwa fedha, lakini amesema Jeshi la Polisi linaendelea na msako kumbaini aliyehusika na uhalifu huo.

Aidha, jeshi hilo limetahadharisha wapenzi na mashabiki wa soka kujihadhari dhidi ya wezi wanaoingia uwanjani kwa nia mbaya huku wakikusudia kufanya uhalifu wakati wa kushangilia ushindi au bao linapofungwa.

Katika mchezo huo Singida United ilipata bao pekee dakika sita za nyongeza kupitia kwa kiungo mshambuliaji, Elinywesia Sumbi, ‘Msingida’ aliyeingia uwanjani dakika ya 78 kuchukua nafasi ya Deus Kaseke.

 Chanzo Nipashe 

Asante Kwasi Amuweka Matatani Kocha Mpya Mfaransa



HUENDA beki wa Simba, Asante Kwasi, akamweka mtegoni kocha wake mpya, Pierre Lechantre, katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa Jumapili hii dhidi ya Majimaji, katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Mtego huo utakaomkumba Pierre utatokana na beki huyo wa Ghana kuwa na majeraha madogo na kushindwa kufanya mazoezi na wenzake na kujifua peke yake kwa mazoezi mepesi, huku akisema ana uhakika wa kupata namba, kwa kuwa majeraha hayo si ya kumfanya ashindwe kucheza.
Juzi katika Uwanja wa Bandari, uliopo Temeke, ambako kikosi cha Simba kinafanya mazoezi yake, BINGWA lilishuhudia beki huyo, Kwasi na Jjuuko Murshid wakifanya mazoezi mepesi tofauti na wachezaji wengine.
Lakini Kwasi aliliambia BINGWA jana kuwa, alifanya mazoezi mepesi kwa kuwa alikuwa na maumivu kwenye mguu, lakini anaamini atakuwa poa na kama kocha na daktari wataruhusu acheze atakuwa tayari.
“Nina majeraha ya mguu, lakini nina uhakika nitakuwa poa kabla ya mchezo wetu dhidi ya Majimaji kama Mungu akijaalia, hivyo kocha na daktari wakiona hali yangu inaruhusu kucheza nitacheza,” alisema Kwasi.
Kwasi ni mmoja wa wachezaji ambao wanaongoza kwa mabao msimu huu wa Ligi Kuu, ambaye anashika nafasi ya tano, akiwa na mabao sita.

Cheki Ya Dozi Ya Azam Ikiandaliwa Vyema Kabisa Na Lwandamina


YANGA wanajua wazi wakikubali kipigo katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam, utakaochezwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Azam Complex, itazima ndoto zao za kutetea taji la ligi hiyo.
Hivyo kutokana na kutokuwa tayari kupoteza taji lao, wamejipanga kuwashangaza Azam kwenye uwanja wao wa nyumbani, huku wakiwa wameandaa wachezaji wenye kasi ya ajabu ‘viberenge’, ili kuwarahisishia mpango wa ushindi.
Wakiwa kwenye mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo wa raundi ya 15, ambao ni wa kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Yanga walipiga tizi katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam na kujifunza mbinu za kupachika mabao wakitumia viberenge hivyo.
Lakini pamoja na mpango wao huo wa kutumia viberenge katika kusaka mabao, pia kocha wa kikosi hicho cha Jangwani, George Lwandamina, alitumia mazoezi hayo kuwaelekeza namna ya kuzuia mashambulizi ya wapinzani wao.
Lwandamina aliwapanga wachezaji Hassan Ramadhani Kessy winga ya kulia na Gadiel Michael winga ya kushoto, kisha kuwapa mbinu mbalimbali jinsi za kupandisha mashambulizi na kuzuia.
Pamoja na maandalizi hayo, lakini Lwandamina alionyesha kufurahishwa na kumalizika adhabu ya kufungiwa mechi tatu mshambuliaji wake, Obrey Chirwa wa Zambia, ambaye katika mazoezi ya juzi na jana alikuwa na morali ya hali ya juu.
Kabla ya kuwapa mbinu hizo, Lwandamina aliwaelekeza nyota hao jinsi ya kupiga krosi za mabao na namna ya kukaba pindi inapotokea wamepoteza mpira langoni mwa adui.

Kocha Wa Maji Maji Atoa Onyo Kali Kwa Mfaransa Wa Simba


KOCHA wa Majimaji, Habib Kondo, amesema hahofii ujio wa kocha mpya wa Simba, Pierre Lechantre, kwani anajua anacheza na Simba ile ile na si mzungu huyo.
Simba na Majimaji wanatarajia kukutana keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na BINGWA jana, Kondo alisema kuwa, wanajua wanakwenda kukutana na timu bora, ila kuhusu suala la kocha mpya, haliwatii presha na kuwafanya waogope mchezo.
Alisema wamekutana na timu ngumu mfululizo, ambazo ni Azam FC na Singida United na kutoka sare ya bao 1-1 kwa michezo yote, hivyo anaamini kikosi chake ni imara.
“Ukiniambia suala la kocha mpya kukabidhiwa timu mimi silifahamu, ninachojua nina mechi na Simba na tumejiandaa kupata pointi muhimu,” alisema Kondo.

Haji Manara Atupa Dongo Jingine Kwa Obrey Chirwa

Katika kile ambacho kinaonekana kuendeleza utani wa jadi, Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara ametupa dongo jingine kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga.
Manara ambaye anajulikana kwa kuwa na maneno mengi ya utani dhidi ya wapinzani wao hao, alitupia mtandaoni picha ya straika wa Yanga, Obrey Chirwa kisha akaweka maneno ya utani kwa mchezaji huyo na klabu yake.
Picha ambayo Manara ameweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, inamuonyesha Chirwa akiwa amejipiga picha kwa staili ya ‘selfie’ huku nyuma yake kukiwa na fundi ambaye anaonekana akirekebisha umeme.
Haji Manara ameandika hivi: “Kama kuna mchezaji ananiacha hoi na swaga zake basi ni @obreychirwa.. kaacha matikiti sasa hivi anaweka umeme, sasa hapo sijui ndiyo Gongowazi walipompangia, nahisi hapo Tandale kwa kinyevule😂😂😂”
Ikumbukwe wiki chache zilizopita, Chirwa alionekana akiwa kwao nchini Zambia akiwa shambani akiendelea na masuala ya kilimo huku upande wa pili timu yake ikiendelea kushiriki katika michuano mbalimbali.
Kipindi hicho Chirwa alikuwa na mgogoro wa kimaslahi na klabu yake, Manara na mashabiki wengine wa Simba walitumia picha hiyo pia kuwatania Yanga mara kadhaa.

Msimamo Wa Kagera Sugar Kuhusu ‘Ishu’ Ya Nyoso

Klabu ya Kagera Sugar imesema haita muadhibu beki wake Juma Said Nyoso ambaye alimpiga shabiki mara baada ya kumalizika mchezo wa ligi kuu tanzania bara kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba Jumatatu Januari 22, 2018.
Inadaiwa shabiki huyo alitoa kauli chafu na za kuudhi kwa Nyoso pamoja na kumpigia kelele za vuvuzela kabla ya Nyoso kuamua kumpiga. Mratibu wa Kagera Sugar Mohamed Husein amema klabu hiyo haitochukua hatua zozote za kinidhamu dhidi ya Nyoso ambaye tayari ameachiliwa kwa dhamana na anaendelea na mazoezi.
“Jambo hili sisi tunaliangalia kwa macho mawili, kwanza tuweke wazi msimamo wetu, sisi hatutompa adhabu yoyote Nyoso kwa sababu yule shabiki alimkosea mchezaji wetu pamoja na Nyoso kuonekana kuwa na tabia ya ukorofi lakini kwa hili yule shabiki alimkosea na mimi nilishuhudia.”
“Kumpulizia mtu vuvuzela kwenye sikio haikuwa sawa lakini wakati huo mchezaji ndio ametoka uwanjani kucheza, lakini shabiki huyo alikuwa akimshabulia Nyoso kwa matusi hata wakati mchezo unaendelea na wakati wa mapumziko bado aliendelea kumtukana sasa na yeye ni binadamu alighadhabika.”
“Shirikisho na polisi wao ndio wataona nini cha kufanya kwa hiyo sisi tunasubiri kuona polisi wataamua nini kama kwenda mahakamani au kumalizana nje ya mahakama sisi tupo tayari. Kijana ameachiwa kwa dhamana na sasa anaendelea na mazoezi na wenzie.”
“Tatizo lililopo kwenye viwanja vyetu vya mikoani si salama sana, njia ambayo wanapita wachezaji kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia mashabiki wanakuwa karibu sana na wachezaji kitu ambacho ni hatari na anamuona huyu ndio ananitukana, sasa kulikuwa na maneno mengi ya kejeli kama unavyojua mechi ile watu walikuwa wanaangalia kati ya Bocco na Nyoso na kelele nyingi zilikuwa kati ya watu hao wawili.”

Evans Aveva Bado Ni Mgonjwa, Amelazwa Muhimbili...





Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, jana alishindwa kuhudhuria mahakamani katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili kwa mara ya pili mfululizo kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa figo akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar.

Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani.

Katika kesi hiyo ambayo iliitwa kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Makahama ya Kisutu, Victoria Nongwa, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Leonard Swai ambaye alikuwa akisaidiwa na wakili wa serikali, Peter Vitalis, aliiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa namba moja, Evens Aveva ameshindwa kufikishwa tena mahakamani hapo kwa kuwa bado ni mgonjwa.

Baada ya Swai kudai Aveva bado anaumwa, hakimu Nongwa alimuuliza anaumwa kitu gani hadi wameshindwa kumfikisha makahamani, Swai alijibu kuwa mtuhumiwa anasumbuliwa na matatizo ya figo na amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Swai aliendelea kusema kuwa pamoja na hivyo, wamekashamilisha upelelezi kwa mshitakiwa namba mbili (Kaburu) baada ya kuomba kwenda kumchukua na kumhoji kwa mara ya pili, hivyo wanasubiria Aveva atoke hospitali ili waweze kuomba kumhoji tena ili kuweza kukamilisha upelelezi.

Kufuatia kauli ya Swai, hakimu Nongwa alilazimika kumuuliza Kaburu kama alihojiwa katika hali ya usalama na taasisi hiyo kwa kuwa hawakumpitisha kwake kuweza kumuona, Kaburu alijibu mahojiano yalikuwa ya amani na mazuri kwani aliweza kufurahia na kuongeza kuwa walimpa hadi chakula cha mchana, hali iliyosababisha watu kuangua kicheko.


Upande wa wakili wa utetezi ambao uliwakilishwa na Peter Warioba aliomba mahakama iruhusu kuendelea na kesi hiyo kutokana na shahadi wa pili kukamilisha  upelelezi lakini halikuweza kukubaliwa na badala yake kesi hiyo imesogezwa mbele hadi Februari 8, mwaka huu itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa tena.

Tambwe Mambo Si Mazuri, Nafasi Ya Kuivaa Azam Fc Kesho Ni Ndogo....



Straika wa Yanga, Amissi Tambwe raia wa Burundi ameshindwa kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake kutokana na majeraha ya goti.


Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu arejee na acheze mechi dhidi ya Mwadui FC kabla ya kuwavaa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar. Mshambuliaji huyo akiwa amekaa nje ya uwanja huku wenzake wakiendelea na mazoezi.

Mshambuliaji huyo, alipata majeraha hayo juzi Jumatano katika mazoezi ya timu hiyo baada ya kugongana na beki wa pembeni, Juma Abdul na kushindwa kuendelea na programu nyingine.

Kutokana na Tambwe kushindwa kufanya mazoezi ya mwishoni ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo, upo uwezekano wa Mrundi huyo kuikosa mechi dhidi ya Azam FC.

Katika mazoezi hayo ya jana, benchi la ufundi la timu hilo, lilionekana kuwaandaa baadhi ya washambuliaji watakaocheza nafasi yake ambao ni Juma Mahadhi na Yohana Nkomola.

Wema Sepetu achoshwa....Atamani Kifo

Muigizaji mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amesema kuna muda anatamani Mungu amchukue afe ili aweze kupumzika na mambo ya dunia ambayo yanamnyima raha.

Wema Sepetu ameyasema hayo kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram, akisema ingawa anajua ipo siku atakufa, lakini anatamani ingetokea sasa ili aweze kupumzika na mambo yanayomuumiza nafsi yake ikiwemo kutukanwa bila sababu za msingi kwenye mitandao ya kijamii.

Wema Sepetu amendeelea kusema kuwa kutokana na mambo ambayo anayapitia anatamani hata asingetokea duniani, na kuamua kukaa nje ya mitandao ya kijamii kwa muda.

"Ipo siku nitakufa, hakuna anaeishi milele... Sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni au ndo itakuwa, “Maskini ya Mungu, Dada wa watu alikuwa hivi na vile, Mungu ailaze Roho yake mahali pema...” Kuna muda mwingine huwa natamani Allah Subhannah wata’allah anichukue tu... Ya Duniya ni mengi sana", ameandika Wema Sepetu.

Wema ameendelea kuandika akisema.." Kuna muda mwingine nakufuru mwenyezi Mungu na kutamani labda hata nisinge exist... Ila acha niendelee kumtegemea yeye... Kila jambo hutokea kwa sababu.... Hili nalo litapita... I think I need a Time Off Social Media... Kwa mara nyingine Tena.... Siwezi jamani".

Licha ya hayo Wema Sepetu hajaweka wazi moja kwa moja ni jambo gani ambalo limemkwaza zaidi, kwani kitendo cha kutukanwa na kusemwa vibaya kwake sio jambo geni. 

Yanga Sc Yakwea Pipa Kufuata Straika Uarabuni

Danny Lyanga.
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wamejitoa kwenye vita ya kumsajili mshambuliaji, Elias Maguli, huku bosi wake akikwea pipa kwenda Uarabuni kwa ajili ya kuvunja mkataba wa Danny Lyanga wa Fanja.

Maguli ni kati ya wachezaji waliokuwepo kwenye mipango ya kusajiliwa Yanga katika usajili huu wa dirisha dogo ambalo limefun­guliwa Novemba 15, mwaka huu.

Lyanga aliwahi kuichezea Coastal Union ya Tanga kabla ya kutua Simba ambako hakudu­mu na kutimkia Urabuni.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, jina la Maguli limeon­dolewa na kamati ya usajili ya timu hiyo katika hatua za mwishoni za kutaka kumsajili.

Mtoa taarifa huyo alisema, kamati hiyo imeliondoa jina la Maguli kwa kigezo kuwa ni mzito na hana kasi ndani ya uwanja na baadaye kuli­pendekeza jina la Lyanga.

Aliongeza kuwa, kamati hiyo ilimfuatilia msham­buliaji huyo na kugundua ana mkataba wa mwaka mmoja na walivyomfuata kuzungumza naye yeye mwenyewe aliku­bali kuongozana na mabosi hao kwa ajili ya kwenda Uarabuni kuvunja mkataba na Fanja.

“Maguli alikuwa chaguo letu la kwanza kumsajili katika majina ya washambuliaji tu­liyoyapendekeza wasajiliwe katika dirisha dogo, lakini baada ya kikao cha mwisho cha kamati tulipokea jina lingine kutoka kwa mwana­kamati mwenzetu.

“Jina hilo ni la Lyanga na kikubwa alikuja na hoja ya msingi kuwa Maguli ni mzito na hana kasi, hivyo basi tumeiona hoja hiyo ya msingi lakini ukaja ugumu mwingine wa Lyanga kuwa bado ana mkataba na Fanja.

“Lakini tulipomfuata Lyanga mwenyewe alikubali kuwa anaweza kusaini na kuongozana na mabosi wa timu hiyo kwenda Uarabuni kwa ajili ya kuvunja mkataba Fanja kama ikiwa sawa basi atakuwa mali yetu lakini ikishindikana bado tutaen­delea kupambana kwa kuwa bado tuna muda,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika kuzun­gumzia hilo alisema kuwa: “Sisi usajili wetu tunaufanya kimyakimya na tuna­tangaza baada ya kukamili­sha kila kitu.

“Na usajili wetu tunaufan­ya kiufundi kwa kumshiriki­sha kocha wetu Lwandamina kwa kufuata mapendekezo yake aliyoyatoa katika timu, hivyo kila kitu kikikamilika ndiyo tunatangaza,” alisema Nyika.

Robinho Akataaa Hukumu ya Miaka Tisa Jela Iliyotolewa na Mahakama ya Itali

Robinho Akataaa Hukumu ya Miaka Tisa Jela Iliyotolewa na Mahakama ya Itali

Baada ya kuhukumiwa miaka tisa jela na mahakama ya Italia kwa kosa la ubakaji, mchezaji wa soka wa Brazil, Robinho amesema hakubaliani na hukumu hiyo kwani hakusika na tukio hilo kama ilivyoelezwa.

“Nimeshachukua hatua zote za kisheria kwaajili ya kujitetea, sikuhusika kwa namna yoyote kwenye tukio hilo kama ilivyodaiwa na tumekata rufaa kupiga hukumu hiyo”, amesema Robinho.
Mahakama ya Italia jijini Milan jana ilimhukumu Robinho pamoja na wanaume wengine watano raia wa Brazil kwenda jela miaka tisa kwa kosa la kumbaka binti mmoja raia wa Albania mwaka 2013. Hata hivyo mahakama imetoa muda kwa Robinho na wenzake kukata rufaa kabla ya kuanza kutumikia kifungo hicho.

Mahakama ilidai kuwa wakati binti huyo anabakwa mwaka 2013 alikuwa na umri wa miaka 22. Tukio hilo linadaiwa kufanyika kwenye club moja ya usiku jijini Milan ambapo Robinho na wenzake walimnunulia pombe nyingi binti huyo na baada ya kulewa ndio wakamfanyia vitendo hivyo.
Robinho mwenye umri wa miaka 33, alicheza AC Milan kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Nyota huyo aliyeanza maisha ya soka kwenye klabu ya Santos ya Brazil pia amewahi kuzichezea timu za Real Madrid na Manchester City. Robinho kwasasa anachezea klabu ya Atletico Mineiro ya Brazil. 

Haji Manara Amwaga POVU Zito Baada Ya LIPULI Kuitwa Tawi La Simba...Atolea Mfano Yanga


Baada ya kuwepo taarifa za kuwepo Undugu kati ya Simba na Lipuli ya Iringa wengi wakiangalia benchi la Ufundi la Lipuli ambalo linaongozwa na Amri Said pamoja na Suleiman Matola huku baadhi ya washabiki wakibeza mechi kati ya Lipuli na Simba kuwa Simba atajichukulia Points 3 bila Ubishi kutokana na benchi lote kuwa la Simba Haji Manara atolea Ufafanuzi.

Akiongea na EFM Haji amekataa kujibu taarifa ambazo zimekuwa zikizuka tu mitandaoni huku akisema suala la Simba kutajwa kuwa na Undugu na Lipuli kisa Amri Said basi watu wanaosema hivyo wahoji pia Kuhusu Afisa habari wa YANGA Dismas Ten kwenda Yanga akitoka kuwa msemaji wa Mbeya City.

Mbona Dismas Ten ametoka Mbeya City kwenda Yanga hamuulizi mnauliza la Amri Said Tu? Mbona hilo hamuulizi, mi najua majawabu yake yapo Mnauliza Swali na mimi nakupa swali he Kwaheri 

Simba itacheza na Lipuli katika mchezo wake unaofuata katika uwanja wa Chamazi siku  ya Jumapili 26.11.2017 wakati Yanga watashuka Dimbani Jumamosi kucheza na Prisons katika uwanja huo huo wa chamazi.

Taarifa Njema Kutoka Yanga…Mashabiki Wa Yanga Lazima Waifurahishe Hii


KLABU ya Yanga ambayo ndiyo mabingwa wa soka nchini jana kupitia kwa katibu wake mkuu wamethibitisha kumalizana na masuala ya Mishahara kwa wachezaji wake jambo ambalo lilikuwa likisemwa sana japo Uongozi wa Klabu hiyo ulikuwa ukilificha.

Mkwasa ambaye ni mchezaji na kocha wa zamani wa Yanga  na sasa akiwa kama katibu mkuu wa Klabu hiyo jana akiongea na EFM amethibitisha kuwa  Wamemalizana na wachezaji waliokuwa wakiwadai mishahara na hakuna mchezaji anayewadai kwasasa na kuhakikisha hilo aliwataka kuwauliza wachezaji wa timu hiyo kama kuna madai ya mishahara.

Na  mmoja wa watangazaji wa Kipindi Alithibitisha kwa kuongea na wachezaji wawili ambao majina yao hawakutaka yatajwe ambao wote walithibitisha kuwa mambo ya mishahara yamekaa sawa.

Kuna taarifa  zilienea siku kadhaa kuwa wachezaji wa Yanga hawajalipwa mishahara ya miezi miwili huku baadhi ya Taarifa zikienda mbali zaidi kwa kusema ni miezi mitatu hawajalipwa ila Taarifa nzuri ni kwamba kila kitu kiko sawa.
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017