Kutokana na mwendo wa kikosi cha Simba katika Ligi Kuu Bara, wengi wanaamini lazima kitabeba ubingwa.
Kocha Msaidizi wa Simba Mrundi, Masoud Djuma ametamka kuwa ni ngumu kutabiri Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kutua Msimbazi katika mzunguko huu wa pili licha ya kuongoza katika msimamo.
Simba hivi sasa inaongoza katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 35 wakifuatiwa na Azam FC wenye 30 huku Yanga wakishika nafasi ya tatu wakivuna 28.
Djuma alisema bado bingwa wa ligi hajaulikana hivi sasa wakielekea kwenye mzunguko wa pili kutokana na kupishana pointi chache dhidi ya wapinzani wao Yanga na Azam.
Djuma alisema, bado wana kibarua kigumu cha kuhakiisha wanashinda kila mchezo utakaokuwepo mbele yao ili waache kwa idadi kubwa ya pointi wapinzani wao.
“Ili tujihakikishie ubingwa wa ligi kuu, basi tunatakiwa kushinda kila mchezo utakaokuwepo mbele yetu bila ya kuidharau hii timu ndogo au kubwa.
“Hilo tumeshwaambia na tunaendelea kuwakumbusha wachezaji wetu katika vikao tunavyovifanya kila siku kabla ya na baada ya mazoezi kwa kuwasisitiza tupambane ili tujiwekee mazingira mazuri ya ubingwa.
“Kama unavyofahamu tumebakisha kombe moja pekee la ligi kuu, kwani tayari tumelipoteza Kombe la FA, hivyo ili tuuchukue Ubingwa wa ligi ni lazima wachezaji wapambane ndani ya uwanja kwa kupata matokeo mazuri ili tuzidi kuwaacha mbali wapinzani wetu Yanga na Azam waliokuwepo chini yetu,”alisema Djuma.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini