Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter
Showing posts with label FASHION. Show all posts
Showing posts with label FASHION. Show all posts

SUMATRA: Marufuku Abiria Kuzungumza Siasa, Dini, Biashara Ndani Ya Basi! ‬


MAMLAKA YA Usimamizi wausafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) imepiga marufuku abiria kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya biashara wawapo safarini.

Agizo hilo limetangazwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Lingadi Ngewe na kwamba abiria atakayebainika kufanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Agizo hilo linakuja baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwapo kwa mvutano wa kupinga kanuni mpya kati ya Sumatra na chama cha wamiliki mabasi yaendayo mikoani (TABOA) na wa usafiri Dar es Salaam (UWAMADAR).

Bila kutaja ni sheria na kanuni ipi, Mkurugenzi huyo amesema ufanyaji wa vitendo hivyo katika mabasi ni kinyume na kanuni za usafirishaji.

"Tutaanza kuzuia wasafiri wa wapo ndani ya mabasi kuacha kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya biashara. Tukibaini hilo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa abiria na dereva ikibidi," amesema na kuongeza

‘Kwa madereva hasa wa kwenda mikoani, njiani wanapandisha wafanyabiashara na kufanya biashara ndani ya basi, hatua kali zitachukuliwa kwa dereva na huyo anayefanya biashara.’

Kimenuka Upya! Soo La Zari, Mobeto Latinga Polisi!

Zarinah Hassan Tiale ‘Zari The Boss Lady’.
DAR ES SALAAM: Hatimaye lile soo baab’kubwa la bifu kati ya mwanamitindo na video ‘vixen’ matata wa Bongo, Hamisa Hassan Mobeto na mwanamama mjasiriamali wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan Tiale ‘Zari The Boss Lady’, limetinga polisi, Risasi Mchanganyiko limetonywa.
KWANI ILIKUWAJE
Sakata hilo linadaiwa kuchukua sura mpya baada ya Hamisa kuundiwa zengwe kwenye mitandao ya kijamii na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wa makosa ya kimtandao.

Zengwe hilo ambalo linadaiwa kufanywa na watu wasiojulikana kwa kujifanya ni wanasheria wa Kampuni ya Danube inayohusika na uuzaji wa fenicha, linaeleza kuwa, mwishoni mwa wiki iliyopita, ilimuandikia Hamisa barua, eti ikimtaka afute posti kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
Video ‘vixen’ matata wa Bongo, Hamisa Hassan Mobeto.
Ilielezwa kuwa, posti hiyo aliyotakiwa kuifuta ni ile inayomuonesha Zari akizozana na mzazi mwenzake juu ya hereni za Hamisa ambazo zilidaiwa kukutwa na Zari nyumbani kwa mwanaume huyo, Madale, nje kidogo ya Jiji la Dar.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Hamisa aliweka ‘clip’ na ‘kuitag’ kwenye ukurasa wa Kampuni ya Danube kisha kusindikizia maneno yaliyosemeka; “Its about time’ nifuate hereni zangu. I hope it’s still there!”
Ujumbe huo ulizua zogo katika mitandao ya kijamii, lakini muda mfupi baadaye, zogo hilo lilihamia kwenye barua iliyosambaa, iliyodaiwa kuandikwa na kampuni moja ya mawakili (jina linahifadhiwa) ikimpa onyo kali Hamisa kuacha kutumia bidhaa zao kwa maslahi yake binafsi.

Kufuatia kasheshe hilo, Risasi Mchanganyiko liliutafuta uongozi wa Danube ili kupata ukweli juu ya utata wa barua hiyo ambapo mmoja wa maafisa wake alifunguka;

“Ninachoweza kusema ni kwamba sisi hatujui chochote kuhusu ujumbe kwa Hamisa, barua inayosemwa imetoka kwetu na zengwe lililoibuka huko mtandaoni.
“Vyote hivyo, ni vitu vipya kwenye macho na masikio yetu. Kiukweli hakuna chochote tunachohusika nacho,” alisema jamaa huyo.


Ofisa mwingine wa kampuni hiyo ambaye naye hakutaka jina lake kutajwa, alisema saini na jina la mwanasheria aliyesaini barua iliyopelekwa kwa Hamisa, siye anayetambuliwa na kampuni yao.

KAULI KUTOKA KWA MAMA MOBETO
Baada ya kusikia kauli hiyo, gazeti hili lilimtafuta Hamisa kupitia simu yake ya mkononi na alipopokea, baada ya kuulizwa kuhusu ishu hiyo, alimtaka mwandishi wetu kupiga baada ya muda kwani alikuwa na kitu anafanya, hata hivyo, alipopigiwa baadaye, simu yake haikupatikana.
Lakini mama yake mzazi, ambaye mara nyingi huongea kwa niaba ya mtoto wake, alisema watu wasifuate sana mambo ya mtandaoni kwa sababu mengi huwa siyo ya kweli.


MAKOSA YA KIMTANDAO HAWA HAPA
Kwa kutambua kuwa, katika sakata hilo kunaweza kuwa na harufu ya kosa la kimtandao, Risasi Mchanganyiko liliwatafuta watu wa kitengo cha Jeshi la Polisi kinachohusika na makosa ya kimtandao kupitia bosi wake aliyejitambulisha kwa jina moja la Joshua.


Katika mazungumzo yake, mkuu huyo wa kitengo alisema bado dawati lao halijapata malalamiko hayo ingawa yeye binafsi amekuwa akiliona tukio hilo mitandaoni.

“Sheria za makosa ya kimtandao ziko wazi, anatakiwa aidha, Hamisa au Kampuni ya Danube ilete malalamiko yao mezani kwetu, sisi tutayashughulikia, ingawa ninaamini kabisa faili hilo tayari litakuwa katika moja ya vituo vya chini likishughulikiwa maana uhalifu huo hata mimi nimeuona,” alisema Kamanda Joshua.

Kauli ya CHADEMA Baada ya Lowassa Kuitwa Polisi Leo Kwa Mahojiano

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa amepata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumanne, saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano.

Mhe. Lowassa ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia CHADEMA, kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, hajapewa maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo yatahusu nini hasa.

Tayari Chama kimetoa maelekezo kwa Kurugenzi ya Katiba na Sheria ya Chama kuhakikisha kuwa Mhe. Lowassa anapata msaada wa kisheria wakati wa mahojiano hayo.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Mhe. Lowassa alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari pamoja na Watanzania wenzetu Waislam waliokuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambapo amekuwa kiitaka Serikali kuzingatia misingi ya utawala bora kama mojawapo ya misingi muhimu ya kuendesha nchi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Watanzania wote.

Imetolewa  Jumatatu, Juni 26, 2017 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Sitti Mtemvu:Kuna Siku Mtaujua Ukweli Kuhusu Umri Wangu

Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amedai sakata la umri lililopelekea kuvuliwa taji la Miss Tanzania ni kitu ambacho kimebadili mfumo wa maisha yake kabisa huku akiwaahidi Watanzania siku moja kuweka wazi ukweli kuhusu umri wake.
Akiongea nasi  wiki hii, Sitti amedai sakata hilo liliweza kubadili mfumo wake mzima wa maisha.
“Mamshukuru Mungu maisha yanaendelea vizuri kwa sababu lile sakata lilikuwa kubwa sana lakini baada ya kumalizika niliamua kurudi shule na namshukuru Mungu nimemaliza salama na sasa anaendelea na shughuli zangu za kawaida,” alisema Sitti. “Ishu ya umri wangu siwezi kuizungumzia kwa sasa tuombe Mungu siku moja nitaanika ukweli na kila mtu anatajua ni nini kilitokea,”
Mrembo huyo kwa sasa anaendelea kufanya bishara ya kitabu chache cha Chozi la Sitti ambacho alikiandika baada ya sakata hilo.
Sitti alisema kitabu hicho kitaweza kuwasaidia vijana wengi hasa wakike katika nyanja mbalimbali za maisha.

Majibu Ya Gigy Money Baada Ya Kuandamwa Kuhusu Kukonda Na Kupoteza Muonekano Wake.


Baada ya kuandamwa na comments kuwa amekonda sana na kupoteza munekano wake, Video model maarufu Tanzania Gigy Money ametoa majibu yake Instagram leo June 2,2017.
Kupitia IG yake Gigy ameandika ”mnakesha kuongeleaaa mwili wangu nimekonda mnaongea nilivyokua kibonge mlikua pia mnanisema aya kwa anaehitaji ninenepe anileteee matunda na vyakula vya mafuta afu mna mind kama kuna mtu nalala nae uku insta kwanza mo j wangu anaupenda huu mwili ananiita katoto sexy basi akisema hivyo nzidi kufanya situps na squats #muachanenamaishayawatumfanyemaishayenu “



Miongoni mwa picha maarufu za zamani za Gigy ilikuwa hii…

Kutana Na Mrembo Mwenye Umbo Matata Kuliko Wote Huko Instagram


 


Kupitia ukurasa wake wa Instagram mrembo huyu amekuwa akiweka picha zake wengi wamekuwa wakimpongeza kuwa ana umbo matata sana wewe unasemaje kwa picha hizi

Hii Ndio Fasheni Mpya Ya Mtoto Wa Barack Obama Itakuacha Mdomo Wazi

Mitindo Hatari Kabisa Ya Nywele Ambayo Ishawahi Kufanywa Na Mstaa Wa Bongo Movie

Irene Uwoya 
  
Wema sepetu

Noma:Wanamitindo Wembamba Wapigwa Marufuku


Sheria nchini Ufaransa inayopiga marufuku wanamitindo wembamba wasio na afya imeanza kutekelezwa.

Wanamitindo watahitajika kuwa na cheti cha daktari kuonyesha afya yao kwa misingi ya vipimo vya uzito wao na kimo.

Wizara ya afya inasema kuwa inataka kukabiliana na matatizo ya kutokula na viwango visivyofikiwa vya urembo.

Mswada wa awali ulikuwa umependekeza uzito na kimo cha wanamitindo hatua iliyopingwa vikali na mashirika ya urembo nchini Ufaransa.

Lakini aina tofati ya mswada ulioungwa mkono na wabunge mwaka 2015 unawaruhsuas madaktari kuamua ikiwa mwamitindo ni mwembamba mno kuambatana na uzito wake umri na mwili.

Waajiri wanaovunja sheria hiyo watapigwa faini ya hadi dola 82,000 au kifungo cha miezi sita jela.
Ufaransa sio nchi ya kwanza kuweka sheria inayohusu wanamitindo wembamba- Italia, Uhispania na Israel washafanya hivyo.
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017