Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Sitti Mtemvu:Kuna Siku Mtaujua Ukweli Kuhusu Umri Wangu

Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amedai sakata la umri lililopelekea kuvuliwa taji la Miss Tanzania ni kitu ambacho kimebadili mfumo wa maisha yake kabisa huku akiwaahidi Watanzania siku moja kuweka wazi ukweli kuhusu umri wake.
Akiongea nasi  wiki hii, Sitti amedai sakata hilo liliweza kubadili mfumo wake mzima wa maisha.
“Mamshukuru Mungu maisha yanaendelea vizuri kwa sababu lile sakata lilikuwa kubwa sana lakini baada ya kumalizika niliamua kurudi shule na namshukuru Mungu nimemaliza salama na sasa anaendelea na shughuli zangu za kawaida,” alisema Sitti. “Ishu ya umri wangu siwezi kuizungumzia kwa sasa tuombe Mungu siku moja nitaanika ukweli na kila mtu anatajua ni nini kilitokea,”
Mrembo huyo kwa sasa anaendelea kufanya bishara ya kitabu chache cha Chozi la Sitti ambacho alikiandika baada ya sakata hilo.
Sitti alisema kitabu hicho kitaweza kuwasaidia vijana wengi hasa wakike katika nyanja mbalimbali za maisha.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017