Klabu ya Kagera Sugar imesema haita muadhibu beki wake Juma Said Nyoso ambaye alimpiga shabiki mara baada ya kumalizika mchezo wa ligi kuu tanzania bara kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba Jumatatu Januari 22, 2018.
Inadaiwa shabiki huyo alitoa kauli chafu na za kuudhi kwa Nyoso pamoja na kumpigia kelele za vuvuzela kabla ya Nyoso kuamua kumpiga. Mratibu wa Kagera Sugar Mohamed Husein amema klabu hiyo haitochukua hatua zozote za kinidhamu dhidi ya Nyoso ambaye tayari ameachiliwa kwa dhamana na anaendelea na mazoezi.
“Jambo hili sisi tunaliangalia kwa macho mawili, kwanza tuweke wazi msimamo wetu, sisi hatutompa adhabu yoyote Nyoso kwa sababu yule shabiki alimkosea mchezaji wetu pamoja na Nyoso kuonekana kuwa na tabia ya ukorofi lakini kwa hili yule shabiki alimkosea na mimi nilishuhudia.”
“Kumpulizia mtu vuvuzela kwenye sikio haikuwa sawa lakini wakati huo mchezaji ndio ametoka uwanjani kucheza, lakini shabiki huyo alikuwa akimshabulia Nyoso kwa matusi hata wakati mchezo unaendelea na wakati wa mapumziko bado aliendelea kumtukana sasa na yeye ni binadamu alighadhabika.”
“Shirikisho na polisi wao ndio wataona nini cha kufanya kwa hiyo sisi tunasubiri kuona polisi wataamua nini kama kwenda mahakamani au kumalizana nje ya mahakama sisi tupo tayari. Kijana ameachiwa kwa dhamana na sasa anaendelea na mazoezi na wenzie.”
“Tatizo lililopo kwenye viwanja vyetu vya mikoani si salama sana, njia ambayo wanapita wachezaji kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia mashabiki wanakuwa karibu sana na wachezaji kitu ambacho ni hatari na anamuona huyu ndio ananitukana, sasa kulikuwa na maneno mengi ya kejeli kama unavyojua mechi ile watu walikuwa wanaangalia kati ya Bocco na Nyoso na kelele nyingi zilikuwa kati ya watu hao wawili.”
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini