Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Haji Manara Atupa Dongo Jingine Kwa Obrey Chirwa

Katika kile ambacho kinaonekana kuendeleza utani wa jadi, Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara ametupa dongo jingine kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga.
Manara ambaye anajulikana kwa kuwa na maneno mengi ya utani dhidi ya wapinzani wao hao, alitupia mtandaoni picha ya straika wa Yanga, Obrey Chirwa kisha akaweka maneno ya utani kwa mchezaji huyo na klabu yake.
Picha ambayo Manara ameweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, inamuonyesha Chirwa akiwa amejipiga picha kwa staili ya ‘selfie’ huku nyuma yake kukiwa na fundi ambaye anaonekana akirekebisha umeme.
Haji Manara ameandika hivi: “Kama kuna mchezaji ananiacha hoi na swaga zake basi ni @obreychirwa.. kaacha matikiti sasa hivi anaweka umeme, sasa hapo sijui ndiyo Gongowazi walipompangia, nahisi hapo Tandale kwa kinyevule😂😂😂”
Ikumbukwe wiki chache zilizopita, Chirwa alionekana akiwa kwao nchini Zambia akiwa shambani akiendelea na masuala ya kilimo huku upande wa pili timu yake ikiendelea kushiriki katika michuano mbalimbali.
Kipindi hicho Chirwa alikuwa na mgogoro wa kimaslahi na klabu yake, Manara na mashabiki wengine wa Simba walitumia picha hiyo pia kuwatania Yanga mara kadhaa.


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017