Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kocha Wa Maji Maji Atoa Onyo Kali Kwa Mfaransa Wa Simba


KOCHA wa Majimaji, Habib Kondo, amesema hahofii ujio wa kocha mpya wa Simba, Pierre Lechantre, kwani anajua anacheza na Simba ile ile na si mzungu huyo.
Simba na Majimaji wanatarajia kukutana keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na BINGWA jana, Kondo alisema kuwa, wanajua wanakwenda kukutana na timu bora, ila kuhusu suala la kocha mpya, haliwatii presha na kuwafanya waogope mchezo.
Alisema wamekutana na timu ngumu mfululizo, ambazo ni Azam FC na Singida United na kutoka sare ya bao 1-1 kwa michezo yote, hivyo anaamini kikosi chake ni imara.
“Ukiniambia suala la kocha mpya kukabidhiwa timu mimi silifahamu, ninachojua nina mechi na Simba na tumejiandaa kupata pointi muhimu,” alisema Kondo.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017