Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Cheki Ya Dozi Ya Azam Ikiandaliwa Vyema Kabisa Na Lwandamina


YANGA wanajua wazi wakikubali kipigo katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam, utakaochezwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Azam Complex, itazima ndoto zao za kutetea taji la ligi hiyo.
Hivyo kutokana na kutokuwa tayari kupoteza taji lao, wamejipanga kuwashangaza Azam kwenye uwanja wao wa nyumbani, huku wakiwa wameandaa wachezaji wenye kasi ya ajabu ‘viberenge’, ili kuwarahisishia mpango wa ushindi.
Wakiwa kwenye mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo wa raundi ya 15, ambao ni wa kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Yanga walipiga tizi katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam na kujifunza mbinu za kupachika mabao wakitumia viberenge hivyo.
Lakini pamoja na mpango wao huo wa kutumia viberenge katika kusaka mabao, pia kocha wa kikosi hicho cha Jangwani, George Lwandamina, alitumia mazoezi hayo kuwaelekeza namna ya kuzuia mashambulizi ya wapinzani wao.
Lwandamina aliwapanga wachezaji Hassan Ramadhani Kessy winga ya kulia na Gadiel Michael winga ya kushoto, kisha kuwapa mbinu mbalimbali jinsi za kupandisha mashambulizi na kuzuia.
Pamoja na maandalizi hayo, lakini Lwandamina alionyesha kufurahishwa na kumalizika adhabu ya kufungiwa mechi tatu mshambuliaji wake, Obrey Chirwa wa Zambia, ambaye katika mazoezi ya juzi na jana alikuwa na morali ya hali ya juu.
Kabla ya kuwapa mbinu hizo, Lwandamina aliwaelekeza nyota hao jinsi ya kupiga krosi za mabao na namna ya kukaba pindi inapotokea wamepoteza mpira langoni mwa adui.


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017