Baada ya kuwepo taarifa za kuwepo Undugu kati ya Simba na Lipuli ya Iringa wengi wakiangalia benchi la Ufundi la Lipuli ambalo linaongozwa na Amri Said pamoja na Suleiman Matola huku baadhi ya washabiki wakibeza mechi kati ya Lipuli na Simba kuwa Simba atajichukulia Points 3 bila Ubishi kutokana na benchi lote kuwa la Simba Haji Manara atolea Ufafanuzi.
Akiongea na EFM Haji amekataa kujibu taarifa ambazo zimekuwa zikizuka tu mitandaoni huku akisema suala la Simba kutajwa kuwa na Undugu na Lipuli kisa Amri Said basi watu wanaosema hivyo wahoji pia Kuhusu Afisa habari wa YANGA Dismas Ten kwenda Yanga akitoka kuwa msemaji wa Mbeya City.
Mbona Dismas Ten ametoka Mbeya City kwenda Yanga hamuulizi mnauliza la Amri Said Tu? Mbona hilo hamuulizi, mi najua majawabu yake yapo Mnauliza Swali na mimi nakupa swali he Kwaheri
Simba itacheza na Lipuli katika mchezo wake unaofuata katika uwanja wa Chamazi siku ya Jumapili 26.11.2017 wakati Yanga watashuka Dimbani Jumamosi kucheza na Prisons katika uwanja huo huo wa chamazi.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini