Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Tunda Fedha za Video Pekee Hazitoshi..Lazima Nijiongeze

MUUZA sura kwenye video mbalimbali za Kibongo, Tunda Sebastian ‘Tunda’ amefunguka kuwa fedha anazolipwa na wasanii wa Bongo Fleva pekee hazitoshi, hivyo anajipanga kutanua kazi zake ili awe wa kimataifa zaidi.

Akichonga nasi, Tunda alisema malengo yake ni kuwa video queen anayekimbiliwa na mastaa wa nje na kupata dili kwa makampuni makubwa ili kuinua kipato chake zaidi kwani fedha pekee anazolipwa na wasanii wa Bongo kwenye video haziwezi kumudu kuendesha maisha yake.

“Ili kuwa bora zaidi nahitaji kutoka kimataifa. Unajua nimekaa sana Bongo, sasa malengo yangu ni kuwashawishi wasanii wa nje kufanya nao kazi ili wanitangaze zaidi kimataifa,” alisema Tunda.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017