Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kwa Hali Yake Ilivyo… wa Kumnusuru Wastara ni Mungu Tu

WA kumnusuru Wastara ni Mungu tu! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia hali ya kusikitisha ya kiafya ya staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma ambayo imekuwa ikizidi kuwa mbaya siku hadi siku.
Tukio bichi lililo kwenye makabrasha ya Wikienda ni la juzi wakati akiwa kwenye maandalizi ya Sikukuu ya Idd ambapo Wastara alipoteza fahamu ghafl a na kusababisha hofu kubwa kwa ndugu, jamaa na marafi ki.
AKIMBIZWA HOSPITALINI
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia wa mwanamama huyo, kufuatia hali hiyo, ilibidi Wastara akimbizwe katika Hosipitali ya Jai Poil ya jijini Nairobi nchini Kenya ambako alikuwa huko kwa ajili ya kazi zake za kisanaa.
Mtoa habari wetu huyo ambaye ni mtu makini aliyefahamika kwa jina moja la Frank alilieleza Wikienda kuwa, yeye na Wastara walikwenda nchini humo kwa ajili ya kazi zao za sanaa ndipo juzi (Jumamosi), akazimia ambapo alikimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.


TATIZO NI NINI?
“Wastara alikuwa akisumbuliwa na mgongo kama kawaida lakini wakati huu hali ilikuwa mbaya zaidi kuliko wakati mwingine wowote ambapo tulikwenda hospitalini, akapewa dawa za maumivu na akawa anatumia na kuwa vizuri kiasi.

“Wakati tukiwa tunaendelea na kazi zetu, ghafl a usiku wa kuamkia Jumamosi, hali yake ilianza kuwa mbaya, huku na huku ghafl a akapoteza fahamu.
“Kuona hivyo, kiukweli tulichanganyikiwa sana, ndiyo tukaamua tumkimbize hospitalini ambapo amelazwa mpaka sasa (juzi),” alisema Frank na kuongeza:
‘TUMUOMBEENI WASTARA’
“Wa kumnusuru Wastara ni Mungu tu kwa sababu amekuwa akipata mateso makubwa. Cha msingi kwa mashabiki wake ni kumuombea kwa Allah, nasi tunaamini atapona ‘soon’ tuendelee na majukumu yetu
kama kawaida.” Baada Frank kuzungumza na Wikienda, mwanahabari wetu
alimtafuta Wastara kwa njia ya simu, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.


Baadaye simu yake ilipokelewa na mtoto wake aliyejitambulisha kwa jina la Tamima na kusema kuwa Wastara hayupo vizuri, yeye ndiye anapokea simu zake.

“Wastara kwa sasa hana hali nzuri, ndiyo maana nimepokea simu yake, iwapo hali yake itakuwa sawa upige baadaye utaongea naye,” alisema Tamima.

MAELEZO YA DAKTARI
Kabla ya kukutwa na mkasa huo wa kusikitisha, hivi karibuni vipimo vya daktari vilionesha kuwa kuna hitilafu kubwa kwenye uti wa mgongo wa Wastara hivyo kushauri kuwa afanyiwe upasuaji wa haraka.

Maelezo ya daktari yalionesha kwamba, Wastara ana tatizo kwenye uti wa mgongo ndiyo maana kwa sasa limeongezeka tatizo lingine la kupoteza fahamu kutokana na uhusiano mkubwa uliopo kati ya uti wa mgongo na mishipa ya fahamu na ubongo.

UPASUAJI NI LAZIMA
Daktari huyo alieleza kuwa, ili kumnusuru Wastara, ni lazima afanyiwe upasuaji wa uti wa mgongo kwa kuwa limeshakuwa tatizo kubwa hivyo kumtaka staa huyo
kutafuta fedha kwa ajili ya matibabu hayo. Hata hivyo, Wastara alipatwa na hali hiyo akiwa kwenye harakati za kutafuta fedha ili afanyiwe upasuaji huo.

Ilielezwa kuwa, Wastara alipata hitilafu kwenye uti wa mgongo tangu kipindi
kile alipopata ajali ya pikipiki akiwa na aliyekuwa mumewe, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambapo ilibidi akatwe mguu wa kulia. Tangu wakati huo, Wastara amekuwa mtu wa kuumwa na kulazwa mara kwa mara ndani na nje ya nchi.

KUTOKA KWA MHARIRI
Wikienda linampa pole Wastara na kumuombea kila la heri ili apone haraka kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu-Mhariri.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017