Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Taarifa Ya Usajili Kuhusu Niyonzima Kusaini Simba Miaka Miwili Hii Hapa…

Baada ya Yanga kumsajisili Ibrahim Ajibu kwa dau nono la shilingi milioni 50 pamoja na kumpa usajifiri wa gari, sasa Simba nao wamejibu mapigo.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa mazungumzo baina ya kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima na Simba yamefikia pazuri.

Niyonzima ambaye amemaliza mkataba wa kuitumikia Yanga hivi karibuni pia alikuwa katika mzungumzo ya kusaini mkataba mpya kuendelea kuichezea Yanga lakini hawakuwa wamefikia kwenye hatua nzuri.
Mtu wa karibu wa Simba ametoa tamko hili baada ya kuulizwa juu ya tetesi hizo: “Ni kweli kaka Niyonzima amesaini Simba miaka miwili kwa dau nono.”

Pamoja na hivyo, rafiki wa karibu wa Niyonzima alipoulizwa juu ya suala hilo, amesema: “Siyo kweli bado hajasaini Simba ila ni kweli alizungumza nao jana.”

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017