Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Katibu Mkuu Wa Chadema Na Viongozi Wenzake Wakamatwa Na Polisi

Viongozi wa Chadema, Picha na Maktaba.

Katibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji, mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na wa Viti Maalumu, Zubeda  Sakuru wamekamatwa na Jeshi la Polisi wilayani Nyasa leo.
Taarifa iliyotumwa leo Jumamosi, Julai 15 kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Mawasiliano cha Chadema, imeeleza kuwa viongozi hao wamepelekwa kituoni kuhojiwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi hao walivamia kikao cha ndani cha Chadema kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Dk Mashinji ya kukagua shughuli za chama katika kanda hiyo.
  • Agosti 30 mwaka jana, viongozi wa Chadema walikamatwa wakifanya mkutano katika Hoteli ya Girrafe jijini Dar es Salaam.
  • Viongozi  waliokamatwa siku hiyo ni Freeman Mbowe, Edward Lowassa, Dk Vicent Mashinji, John Mnyika na Said Issah, ambao walikuwa wakikutana na jumla ya wajumbe 170 wa chama hicho.
Tutaendelea kuwajuza kuhusu tukio hili

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017