Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Mama Kanumba Ashindwa Kula, Kisa ‘Kifo Cha Ramsey’


MAMA wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka kuwa, kufuatia taarifa za Mwigizaji wa Nigeria, Ramsey Noah kuzushiwa kifo, alijikuta akipata mshtuko na kushindwa kula kwa kukumbuka maneno aliyowahi kumwambia mwanaye kipindi cha nyuma.

Ramsey Noah.
Mama Kanumba aliliambia Wikienda kuwa, siku chache zilizopita watu mbalimbali walikuwa wakimpa taarifa kwamba msanii huyo amefariki dunia na kujikuta taaban baada ya kukumbuka kauli ya Ramsey aliyewahi kumwambia Kanumba kwamba sanaa imejaa ushirikina hivyo ajikite kwenye maombi.
n




Kanumba enzi za uhai wake.
“Ile ishu ilinipa wakati mgumu, niliapa lazima nikamzike kutokana na ukaribu aliokuwa nao kwa marehemu Kanumba, ile kauli yake nilivyoikumbuka ndiyo iliniumiza zaidi nikakosa nguvu kabisa, ikabidi nipige simu kwa watu wangu kujua kama ni kweli amekufa hadi nilipothibitisha ni uzushi ndiyo nikawa sawa,” alisema Mama Kanumba.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017