Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Yaliyojiri Kortini Kesi Ya Kutumia Dawa Za Kulevya Inayomkabili Masogange

Agnes Gerald ‘Masogange’ alivyofikishwa kortini

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Julai 13, 2017 imekwama kuanza kusikiliza kesi kuhusu kutumia dawa za kulevya inayomkabili video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kwa sababu ana tatizo la kiafya.

Wakili wa serikali, Constantine Kakula, amedai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa kesi hiyo leo ilikuwa ianze kusikilizwa.

Hata hivyo, wakili wa Masogane, Ruben Simwanza, alimweleza hakimu kwamba mteja wake anaumwa hivyo anaomba kesi iahirishwe. Hakimu Mashauri alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi July 25, 2017.

Masogange anashtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni kutumia dawa za kulevya aina ya Heroine na Oxazepam  na Heroine (Diacety Imophine).

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017