
Edward Lowassa na Lazaro Nyalandu.
ALIYEKUWA Mgombea Urais wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassaamemkaribisha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye amejivua uanachama na kuachia nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Lazaro Nyalandu (47), aliyekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango ambapo dakika chache baadaye Lowassa alimkaribisha waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii huku akisema mbona mwanasiasa huyo amechelewa kujiunga na upinzani.
“Mbona amechelewa? Alitakiwa awe amejiunga muda mrefu, tena hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ninamkaribisha sana kwa sababu ni mwanasiasa mzuri na anayejua majukumu yake. Nyalandu ni hazina, ni mbunge imara na ni mwanasiasa wa mfano,” alisema Lowassa.
Lowassa amemsifu Nyalandu kwa kuisaidia jamii na akatoa mfano jinsi alivyosaidia watoto watatu wa Shule ya Lucky Vincent waliokwenda kutibiwa Marekani baada ya kupata ajali ya basi iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja wilayani Karatu. “Nyalandu ana contacts nyingi na jumuiya ya kimataifa, ni bidhaa nzuri kuwa nayo,” alisema Lowassa.
Nyalandu pia alifanya jitihada za kutaka kumsafirisha Mbunge mwenzake, Tundu Lissu kwenda nje ya nchi kutibiwa baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa licha ya madaktari kueleza kuwa bado anaweza kuendelea kutibiwa Nairobi Hospital.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini