
- Tikiti maji ni moja wapo ya tunda ambalo ni muhimu sana katika mwili wa binadamu kwani lina nguvu ya ajabu ya kuweza kutibu magonjwa mbalimbali na kuufanya mwili wako kuwa na afya ambayo inatakiwa, tunda hili lina asilimia 92 ya maji na madini, mara nyingi ni chaguo zuri kwa wagonjwa wenye upungufu wa maji mwilini.
- Upatikanaji wa aina hii ya tunda ni rahisi sana kwenye jamii yetu na hata gharama za kulimudu pia sio za juu sana.
- KURAHISISHA MMENG’ENYO WA CHAKULA.
Tikiti maji ni tunda muhimu katika kurekebisha mmeng’enyo wa chakula Kwa kuwa tunda hili limetengenezwa na kiasi kikubwa cha maji na fiber ambazo husaidia kuondoa matatizo ya kukosa choo na kuboresha mmeng’enyo wa chakula tumboni.
HUSAIDIA MISULI NA MISHIPA.
Kutoka na utajiri wake wa madini ya potassium husaidia sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, na uanzishaji wa mwendo katika misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari na husababisha mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na msukumo wa damu mwilini.
KUNG’ARISHA NGOZI.
Tikitimaji husaidia afya ya ngozi kwa kuwa lina vitamini A na C; Vitamini A husaidia katika ukuaji wa tishu za mwili zikiwemo ngozi na nywele hukuVitamini C ikisaidia katika utengenezaji wa kolageni mwilini na husaidia kupona haraka kwa tishu zilizo na majeraha ikiwemo ngozi.
KUIMARISHA MISHIPA YA MOYO NA MIFUPA.
Virutubisho (lycopene) vinavyopatikana kwenye tikiti maji ni mahususi kwaajili ya moyo pamoja na mishipa yake lakini hivi karibuni imegundulika kuwa virutubisho hivyo pia huimarisha mifupa yetu.
Ulaji kwa wingi wa tikiti maji husaidia mzunguko wa damu kuzunguka vizuri bila matatizo yoyote. Na pia husaidia kupunguza msongo wa mawazo ambao mara nyingi hupunguza kasi ya ufikiriaji mzuri, wakati huohuo madini ya potassium yanayopatikana katika tikitimaji husaidia kuimarisha mifupa ya mwili na kuifanya kuwa imara na yenye nguvu.
- HUSAIDIA KUONDOA/KUPUNGUZA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME
Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake na mbegu zake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini