Wakati mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe akiwa ameanza mazoezi mepesi tangu jana Jumanne, kiungo Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi naye ameanza mazoezi mdogomdogo.
Yanga imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Mbeya City, Jumapili ijayo.
Tambwe ambaye hajacheza kabisa msimu huu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti, alikuwepo uwanjani akikimbia na kunyoosha viungo kama ilivyokuwa kwa mwenzake Tshishimbi.
Majeruhi mwenzake, kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko hakuwepo kabisa na hatarajiwi kucheza katika mchezo wa wikiendi hii.
Daktari wa Yanga, Edward Bavu amesema mchezaji huyo wa zamani wa Mbabane Swallows ya Swaziland anasumbuliwa na homa ya Malaria.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini