Mahakama ya Juu nchini Kenya leo jumatatu tarehe 20 Novemba 2017, imetupilia mbali kesi mbili zilizokuwa zimewasilishwa kupinga uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu, Uchaguzi ambao ulimtangaza Rais Uhuru Kenyatta kuwa mshindi.
Jaji Mkuu nchini Kenya, David Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kuwa Kesi ya Bw. Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif za kuweka pingamizi juu ya ushindi wa Rais Kenyatta zimetupiliwa mbali.
“Uchaguzi wa 26 Oktoba ulifanyika kwa usawa na ulidumishwa hivyo Kenyatta alishinda kwa uhalali, Kila upande utasimamia gharama yake.” amesema Jaji Maraga.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa urais kwenye marudio ya Uchaguzi akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98% ya kura zote zilizopigwa.
Uchaguzi ambao ulisusiwa na kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya, Raila odinga akitaka Tume ya Uchaguzi nchini humo IEBC ifanyiwe mabadiliko.
Wapiga kura milioni 7 sawa na asilimia 38.8 kati ya watu milioni 19.6 ambao walijiandikisha kupiga kura nchini humo walishiriki uchaguzi huo.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini