Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

EPL Yatisha Orodha Ya Timu 10 Zinazolipa Zaidi Barani Ulaya

Pesa imeingia kwenye soka, vilabu vinatumia kiasi kikubwa sana cha pesa ili kujiimarisha na ndio maana kwa soka la sasa sio kitu kigumu kwa mchezaji kuuzwa £200m, orodha ya klabu zinazolipa zaidi barani Ulaya imetoka.
Orodha ya vilabu ambavyo vinatumia kiasi kikubwa sana kulipa mishahara imetoka huku timu za Epl zikichukua nafasi kubwa katika orodha hiyo.
10.Juventus, wako katika nafasi ya 10 ambapo wanatoa kiasi cha £150m katika malipo yao, katika klabu hiyo anayeongoza kwa kupokea mshahara mkubwa ni Gonzalo Higuain anayepokea £130,000 kwa wiki.
09.Liverpool. Wako nafasi ya 9 katika orodha hii ambapo wanalipa kiasi cha £210m huku Phelipe Coutinho akiwa anaongoza kupokea mshahara mkubwa (£200,000) kwa wiki.
08.Arsenal, baada ya kuongeza nyota wakubwa akiwemo Alexandre Lacazette sasa klabu ya Arsenal wanatoa karibia kiasi cha £201m ambapo mchezaji anayepokea zaidi katika klabu hiyo ni Mesut Ozil anayepokea £150,000 kwa wiki.
07.Bayern Munich. Roberto Lewandoski ndio mchezaji anayeongoza kwa kupokea mshahara mrefu Bayern Munich anakula £160,000 kwa wiki huku Bayern wakitoa jumla ya £235m kila msimu.
06.Real Madrid. Madrid walipunguza mzigo kwa kumtoa Alvaro Morata na Danilo na sasa Los Blancos wanatoa kiasi cha £240m huku Cr7 akiweka mfukoni kiasi cha £365,000 kwa wiki.
05.Manchester City. Sergio Aguero anapokea £220,000 kwa wiki huku matajiri hao wa Uingereza wakiwa wanatoa kiasi cha £244m kwa wachezaji wao hii ikichagizwa na ongezeko la nyota wengi wakubwa akiwemo Kyle Walker na Danilo.
04.Chelsea. Eden Hazard anapokea kiasi cha £200,000 kwa wiki na ongezeko la Tiemoue Bakayoko na Alvaro Morata linawafanya kutoa kiasi cha £250m.
03.Manchester United. United wako juu ya majirani zao City na Paul Pogba anaongoza kwa kupokea Man City ambapo anapokea kiasi cha £290,000 kwa wiki huku United wanatoa £264m, Pogba alianza kulipwa ghali tangu anawasili lakini ujio wa Romelu Lukaku umezidi kuifanya United kutumia pesa kubwa katika mshahara.
02.Barcelona. Lioneil Messi anaongoza kwa kupokea mshahara akiwa anaweka mfukoni £500,000 kwa wiki huku kwa ujumla Barcelona wanatoa £264m, pamoja na kuondoka kwa Neymar lakini ujio wa Dembele na uwepo wa nyota wengine kama Suarez na wengineo bado unawafanya Barca kulipa pesa nyingi.
01.Paris Saint German. Haishangazi PSG kuwepo katika nafasi ya kwanza, kwani uwepo wa mastaa wakubwa kama Kylian Mbappe, Edison Cavanni kunawalazimu watoe pesa nyingi (£279m) huku Neymar akipokea £537,000 kwa wiki.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017