Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kakolanya Kuondoka Yanga? Ishu Nzima Ipo Hivi



Golikipa wa Yanga Beno Kakolanya amethibitisha kutaka kuondoka katika klabu hiyo, baada ya kushindwa kumlipa mshahara wa miezi mitatu huku akiwa
anadai fedha za usajili Sh milioni 11.

Amesema mpaka sasa yeye ni mchezaji huru, baada ya Yanga kushindwa
kumlipa fedha zake za usajili na mshahara wa miezi mitatu na kwa mujibu wa mkataba wake.
Baaada ya taarifa hizo katibu mkuu wa klabu hiyo Boniface Mkwasa alizijibu kuwa wao hawawezi kumnyima mshahara wake cha muhimu avumilie.

"Hakuna sababu yoyote ya sisi kumnyima mshahara wake, kwani wangapi wanadai?, inabidi avute tu subira tu, tutamlipa mambo yakikaa sawa" hayo ameyasema Mkwasa akizungumzia madai ya Beno Kakolanya ambaye anaidai klabu ya Yanga alipozungumza na SportsExtra- CloudsFM

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017