Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kamati Ya Bunge Yawaweka Kitimoto Waandishi Wa Habari

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imewahoji wahariri pamoja Waandishi wa Habari wa Magazeti ya Mtanzania, Mwananchi na Nipashe kwa kosa  la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya Bunge.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Almasi Athuman Maige (Mb) ambapo amesema kuwa wahusika wote walifika mbele ya Kamati na kujibu tuhuma hizo ambazo ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f)  na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Maige amesema kuwa Kamati baada ya kuwasikiliza mashahidi wote waliofika itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kwaajili ya hatua zingine za kinidhamu..
“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa Bungeni,” amesema Maige
Hata hivyo, amewataja waliofika katika Kamati hiyo kuwa ni Denis Msaki ambaye ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania na mwandishi wake, Bakari Kimwanga, Ndugu Edmond Msangi Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe na mwandishi wake, Gwamaka Alipipi na Ndugu Angetile Osiah Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi  na Mwandishi wake, Elias Msuya.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017