Wachezaji wa Yanga na Simba mchezo ukiendelea.
KAMATI ya Saa 72 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inatarajia kukutana wakati wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kujadili madai ya Simba kunyimwa penalti katika mechi kadhaa ikiwa ni pamoja na mambo mbalimbali yaliyojitokeza katika mechi za hivi karibuni.
Simba kupitia msemaji wake, Haji Manara wamelalamika juu ya waamuzi kuwadhurumu kwa kutowatendea haki katika mechi tatu kwa kuwanyima na kutoa penalti ambayo si halali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Salum Chama amesema madai ya Simba yatafikishwa katika Kamati ya Saa 72 ili kupitia mechi husika kama ilivyo taratibu walizojiwekea.
“Manara ametumia haki yake ya msingi kusema vyovyote anavyojisikia kwa mujibu wa kanuni na sheria ya nchi ilimradi asivunje sheria.
“Sisi kama kamati ya waamuzi tunaona waamuzi wetu wanachezesha sawa kwani kwenye soka kuna kushinda, kufungwa na kutoa sare, hoja ya kunyimwa penalti siyo kweli, na si kila mpira unaompiga mchezaji ni penalti, mwamuzi ndiye anayeamua.
“TFF ina kamati watapitia vipande vya video za michezo inayolalamikiwa na kuangalia maeneo yote yenye matatizo katika mechi zilizochezwa na iwapo tutabaini upungufu wowote tutachukua hatua kwa mujibu wa kanuni tuliyojiwekea katika kamati yetu,” alisema Chama.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini