Mlinzi wa kati wa mabingwa watetezi wa Ligi kuu soka ya Tanzania Bara VPL Yanga Kelvin Yondani yupo katika hati hati ya Kuukosa mchezo kati ya Yanga na Mbeya City mara baada ya kuumia kifundo cha mguu akiwa Timu ya Taifa.
Yondani aliumia kifundo cha Mguu akiwa na timu ya Taifa walipocheza mechi ya kirafiki Ugenini Benin katika mchezo ambao uliisha kwa bao 1 kwa 1.
Yondani amekuwa Mlinzi muhimu sana Yanga na amekuwa akicheza karibu mechi zote kasoro mchezo mmoja pekee wa Ligi uliozikutanisha Stand United na Yanga nafasi yake ikizibwa vyema na Mlinzi mkongwe Nadir Haroub Cannavaro.
Hata hivyo mtandao huu wa Kwataunit.com unasubiri majibu ya Mwisho kutoka kwa daktari wa Yanga Dr. Edward Bavu kuthibitisha kama mchezaji huyo atakosekana ama la.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini