Kwa mujibu wa Gakwaya Olivier ambaye ni Afisa Habari wa klabu ambayo alikuwa akiitumikia Ndikumana kabla ya mauti, Rayon Sports ya Rwanda, amesema muda mfupi uliopita kwamba Ndikumana ambaye alikuwa kocha wao msaidizi amefariki kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni ugonjwa wa moyo.
.
“Alisikia maumivu makali kifuani akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza kunywa tu kidogo akatapika na akaishiwa pumzi na ndipo akakata kauli,” alisema Olivier na kuongeza kwamba bado wanasubiri uchunguzi wa kina wa kitabibu. R.I.P Ndikumana
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini