Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Lema Amjibu Mange Kimambi Kuhusu Uchaguzi Wa Madiwani

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (kulia) na Mange Kinambi.
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amemtoa wasiwasi mwanadada anayefahamika kama mwanaharakati wa mitandaoni,  Mange Kimambi,  kwamba asijali kwani wananchi watatoa maamuzi juu ya kilichotokea kwenye uchaguzi mdogo Jumapili iliyopita.
Lema amelazimika kumuondoa wasiwasi mwanadada huyo baada ya kuonyesha hisia za hasira kwa viongozi wa upinzani ambao wamekuwa wakilalamika kufanyiwa madhamibi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akiwataka wachukue maamuzi magumu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange amewaambia viongozi wa upinzani kutoa majibu ya kilichofanyika kwenye uchaguzi wa madiwani na kuchukua hatua kuliko kukaa na kulalamika huku wakiwakatisha tamaa wanachama wao.
Baada ya maoni marefu ya  Mange aliyoyaandika, Lema amemjibu mwanadada huyo kwamba:
“Mange, nimekusoma/ nimekuelewa watu wana hasira kuhusu mambo yanoyoendelea nchini hususani ktk uchaguzi huu wa marudio ya udiwani, kelele juu ya dhuluma hizi ni muhimu, acheni kwanza watu wote wajue kilio chetu, maamuzi ya dhati yatatoka kwa wananchi. Only Time will tell. Usiogope” Lema.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017