MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema kisasi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchukua wanachama wake kitasaidia kuwaondoa wavulana kwenye mapambano ya siasa za upinzani.
Lema ameyasema hayo ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Patrobas Katambi, kuomba ridhaa ya kujiunga na CCM katika kikao cha Halmashauri Taifa.
Mbunge huyo amesema bado kuna mameya wawili ambao watakihama Chadema, ikiwa ni pamoja na kijana mmoja aliyekuwa shupavu katika chamahicho katika kipindi cha kati ya mwaka 2010 na 2015.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Vicent Mashinji, amesema kwamba: “Ni muda wa kutofautisha kati ya wanaume na wavulana! Wana CHADEMA msihofu tunazidi kuimarika. Kila abiria atashuka kwenye kituo chake lakini safari ya ukombozi inaendelea.”
Hata hivyo juhudi za kumtafuta Lema kwa ajili ya kumtaja jina kijana huyo anayetarajiwa kuondoka Chadema hazijazaa matunda kwani simu ya Mbunge huyo haikupokelewa.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini