Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

MAAJABU:: Tajiri Bongo Ajiandalia Kaburi Kubwa La Mamilioni..Tazama Picha Zaidi

Mganga wa tiba asili maarufu ‘dokta’ Antony Mwandulami.

IRINGA:Mshangao! Mganga wa tiba asili maarufu ‘dokta’ Antony Mwandulami, mkazi wa kijiji cha Itunduma Wilaya ya Njombe mkoani Iringa ametoa mpya ya kufuru baada ya kuamua kujenga eneo la makaburi yake na wake zake watatu ambayo yakikamilika, yatakuwa yamegharimu kiasi cha shilingi bilioni moja.
Akizungumza na Uwazi, Mwandulami alisema ameamua kujenga kaburi hilo kwa lengo la kuweka kumbukumbu kwa jamii yake, familia na hata kazi yake ya utabibu akiwa na wake watatu na watoto kumi na tisa.
Nyumba yake.
Akizungumzia juu ya kaburi hilo na ujenzi wake, mwandulami alisema litakuwa kama nyumba, ambayo imechimbwa chini ambako kumegawanywa sehemu yenye maeneo manne.
“Ukubwa wa kaburi langu ni heka moja, kwani nimejenga ngome kubwa na ndani yake ndiyo kuna eneo la kaburi lililoko chini ya ardhi. Eneo la kaburi ni kubwa kwa sababu kutakuwa na maeneo tofauti” alisema.
“Ninataka kutunza kumbukumbu za kazi zangu ambazo nimezifanya kwa muda mrefu, sitaki jina langu lipotee, hivyo nataka kutengeneza kaburi la kipekee” alifafanua dokta huyo.
“Hili kaburi nimeanza kulijenga kwa miaka tisa sasa, ninategemea kulimaliza mwaka 2018 kwa gharama ya shilingi bilioni moja. Kwa sasa nimefikia hatua nzuri ya ujenzi, kilichobaki ni kufanya ‘finishing’ tu.
Gari lake.
Kaburi moja lina sehemu nne
Alisema kwenye nyumba hiyo ambayo ni kaburi kuna jumla ya makaburi manne, kaburi moja litakuwa lake na mke wake mkubwa lakini pia kuna sehemu nyingine kutakuwa kuna kaburi la wake zake wawili.
“Kama ambavyo nilivyosema awali, nataka kuacha kumbukumbu, kwa hiyo ili kufika kwenye kaburi langu, kuna sehemu ya mapokezi, na sehemu zingine za kupumzika kwa wageni watakaotembelea kaburini ambalo liko kiasi cha mita 30 chini ya ardhi,” alisema.
Kaburi lake.
“Ninaagiza marumaru mbalimbali kutoka Sweden kwa ajili ya kumalizia makaburi hayo. Hizi zitasaidia kutunza mwili wangu kwa muda mrefu ili vizazi na vizazi waweze kuniona na kujifunza kwa huduma nilizokuwa nazitoa wakati wa uhai wangu” alijigamba dokta huyo.
“Watanzania wana woga sana katika kuzungumzia suala la kifo, lakini mimi na wake zangu tumezungumza na wameridhia na kubariki ujenzi huo wa kaburi letu,” alimalizia mtabibu huyo.
-GPL

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017