Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John
Pombe Magufuli amewaonya wanachama wapya ambao wamehamia ndani ya chama hicho
leo kwenye mkutano mkuu wa NEC unaoendelea Ikulu jijini Dar es salaam.
Wanachama hao ambao wamehamia
na kutangazwa leo ni Mwanasheria Alberto Msando aliyekuwa mwanachama wa
ACT-Wazalendo, Mbunge wa zamani wa Nyamagana Laurent Masha aliyekuwa mwanachama
wa Chadema pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema taifa Patrobas
Katambi.
Wengine
ni Profesa Kitila Mkumbo ambaye naye alikuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo pamoja
na Sophia Simba ambaye ameomba kurejeshewa uanachama baada ya kufukuzwa kwa
muda.
Akiongea baada ya kuwapokea
wanachama hao Rais Magufuli amesema, “Nawaomba msije mkabadilika tena, mmekuja
huku na wanachama wamewakubali msirudi tena kule, hiki ni chama cha wote hata
watoto watazaliwa watakikuta na watajiunga kwasababu kina misingi imara,
kwahiyo msije huku kujaribu”.
Rais
Magufuli amemaliza kwa kuwapa ruhusa ya kugombea nyadhifa mbalinmbali ndani ya
chama na kwenye maeneo yao. “Nyie sasa mmepitishwa na mkutano mkuu wa NEC
hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuwapinga na kama kuna nafasi ya kugombea
huko nendeni mkagombee ili mje mshiriki kuijenga nchi na Chama”.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini