Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

MASHABIKI WA CHELSEA MPOO:: DK Shika Asema Yeye Ni Shabiki Wa Chelsea, Atoa Sababu Hii Ya Kuipenda Chelsea

DK SHIKA 

Dk Louis Shika ambaye amekamata vichwa vya vyombo vya habari baada ya uamuzi wake wa kuzinunua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi, amesema anapenda michezo lakini si kihivyo sana.

Katika michezo anayoipenda, Dk Shika amesema kuwa anashabikia zaidi soka la England na timu inayomvutia ni Chelsea.

Shika ametuambia  kwamba anaupenda mpira na uamuzi wake wa kuishangilia Chelsea ni kwa kuwa inamilikiwa na rafiki yake.

Shika amesema Chelsea inamilikiwa na Roman Abramovich, bilionea raia wa Russia ambako Dk Shika alipata elimu yake ya udaktari.

“Napenda michezo na soka ndiyo zaidi. Timu za nje ndiyo napenda zaidi mpira wao, nashangilia sana Chelsea.

“Unajua mmilili wake (Abramovich) ni rafiki yangu,” alisema.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017