Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, ameendelea kusisitiza kwamba yeye bado ni kiongozi halali wa nchi hiyo na kukataa upatanishi unaofanywa Kasisi mmoja wa Kanisa Katoliki ili kuwezesha mabadiliko ya uongozi kwa njia amani baada ya jeshi kuchukua.
Rais Mugabe
Taarifa zaidi za kiintelijensia zinadai, Makamu wa Rais aliyetimuliwa, Emmerson Mnangagwa, amekuwa akiandaa mpango wa uongozi baada ya Mugabe kuondoka madarakani akishirikiana na jeshi pamoja na upinzani kwa zaidi ya mwaka sasa.
Wakati huo huo, kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC, Morgan, Tsvangirai, ambaye amekuwa akipatiwa matibabu ya Saratani nchini Afrika Kusini na Uingereza amerejea Zimbabwe jana.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini