Licha ya Brazil kuifunga Japan mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki upande mwingine kukaibuka kitu cha kushangaza kuhusu staa wa Brazil, Neymar.
Neymar akiwa katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, alianza kulia na kuamua kuondoka kwenye mkutano wake huo baada ya kuulizwa maswali kuhsu kuwa na tofauti kati yake na kocha wake wa Brazil pamoja na staa wa PSG, Edison Cavani.
Neymar aliangua kilio wakati kocha wake, Tite akimzungumzia na akimtetea kuhusu habari zinazoandikwa siku za usoni kwamba hana furaha na maisha ya PSG na uhusiano wake na kocha wa klabu hiyo sio mzuri.
Tite amesema anakerwa sana na habari anazozishiwa Neymar ikiwemo kuwa na mahusiano mabaya na yeye kwani hajawahi kugombana na Neymar, wakati Tite akiendelea kumtetea Neymar ndipo alianza kulia.
Neymar mwenyewe kabla ya Tite kuongea alisisitiza kwamba ana furaha kuwa katika klabu ya PSG na kusema kwamba hana tatizo na mchezaji yoyote katika klabu hiyo, na yuko vizuri tu na Edison Cavani.
Alisisitiza kwamba kitu pekee kinamsumbua kwa sasa na kuambiwa hayuko vizuri na Edison Cavani na amewataka waandishi wa habari kuacha kutunga story na kuandika vitu wasivyovijua.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App Yetu
Android ===> Bofya hapa
Neymar alisajiliwa na PSG akitokea Barcelona kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia ya pauni 198m lakini tangu atue PSG amekuwa akitengeneza vichwa vingi vya habari na vingi vikiwa sio vizuri.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini