Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Samba Na Azam Zaingia Katika Vita Nzito Ya Kumuwania Straika Huyu Hatari


Wakati timu na makocha wakiumiza vichwa juu ya nani wa Kuongeza na kupunguza katika dirisha dogo lengo likiwa ni kuboresha vikosi kuelekea VPL na Michuano mingine kitaifa na Kimataifa Imeibuka vita ya chini chini kati ya Azam na Simba.


Taarifa ambazo mtandao wetu wa Kwataunit.com tumezipata ni kwamba Azam wamemtuma mtu nchini Zambia kwenda kumalizana na Mchezaji Zambia, Moja kati ya majina yanayotajwa kuwa Azam wameyafungia safari ni Chrispin Mugalu lakini mwingine ni yule ambaye siku mbili tatu amekuwa akitajwa kuwindwa na Simba kwa muda sasa Walter Bwalya.


Mpaka sasa Uongozi wa Azam umegoma kabisa kusema ni mchezaji gani wanayemtaka Kumuongeza ila wamesema tu Atatoka kati ya Zambia ama Ghana ila wamegoma kabisa Kumtaja wakati mchezaji mwenyewe Walter Bwalya akisema yuko tayari kucheza timu yoyote ile kama dau litasomeka vizuri.


Bwalya kwasasa anacheza katika klabu ya Nkana ya huko kwao Zambia na Simba wamekuwa wakidaiwa kumsaka toka kipindi cha Usajili ila ilidaiwa msomaji wa Kwataunit.com kuwa alitaka Dau kubwa sana kwa wakati huo.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017