Klabu ya Simba ambao ndiyo vinara wa Ligi kuu wakiwa na Points 22 kwenye msimamo wa Ligi Kuu VPL wamezungumza kuhusiana na wachezaji wake wawili wa kimataifa kutoka Uganda Juuko Murshid na mshambuliaji wao Emmanuel Okwi mara baada ya wachezaji wake hao kukosekana katika mchezo kati ya Prisons na Simba.
Afisa Habari wa Klabu ya Simba Haji MANARA amesema
"Okwi aliumia kwenye mechi dhidi ya Mbeya city hata Uganda alienda tu kwakuwa tiketi yake ilifika mapema kabla ya mechi ya Mbeya City kwahiyo ameshapona na kesho ataanza mazoezi, Juuko naye aliumia lakini yupo na kesho wote wataanza Mazoezi."
Simba msomaji wa Kwataunit.com leo wanatarajia kuendelea na mazoezi hii leo baada ya jana kuwa na Mapumziko wakijiandaa na mchezo dhidi ya Lipuli wikiendi hii katika uwanja wa Uhuru kabla ya Ligi kusimama kupisha michuano ya CECAFA Challenge Cup.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini