Round ya 9 ya game za Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 imeendelea leo kwa Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Dar es Salaam Young Africans dhidi ya Singida United katika uwanja wa Namfua mkoani Singida.
Yanga wakiwa ugenini wameendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo wa ugenini msimu wa 2017/2018 na leo wamecheza game yao ya tano ugenini dhidi ya Singida na kuambulia sare tasa (0-0), hiyo ikiwa game yao ya pili ugenini kupata sare wakiwa wameshinda game tatu.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App Yetu
Kwa matokeo hayo sasa Yanga wanakuwa wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na jumla ya point 17 sawa na Mtibwa Sugar wakipishana kwa tofauti ya magoli, kesho ni zamu ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini