Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Sophia Simba Arejeshwa Ccm Baada Ya Kuomba Radhi

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake CCM (UWT), Sophia Simba.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake CCM (UWT), Sophia Simba aomba radhi na kuomba kurejea CCM baada ya kufukuzwa uanachama.
Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli amesoma barua ya Sophia kuomba radhi mbele ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na kuwahoji wajumbe kama wanakubali kumsamehe jambo lililokubaliwa.
“MwanaCCM aliyefukuzwa uanachama amekuwa akiandika barua nyingi za kuomba radhi lakini tumekuwa tukinyamaza,  kikao hiki ndiyo kilimfukuza,” amesema Rais Magufuli katika kikao hicho kinachofanyika leo Jumanne.
Baada ya kuwahoji wajumbe na kukubaliwa Rais Magufuli aliandika kwenye barua hiyo kuwa amekubaliwa kurudi CCM.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017