Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Tp Mazembe Yakaribia Kutwaa Ubingwa Wa Kombe La Shirikisho Afrika

Fainali ya kwanza ya mchezo wa shirikisho Africa imepigwa hii leo mjini Lubumbashi ambapo wenyeji Tp Mazembe wakiwa nyumbani waliikaribisha klabu ya Super Sport kutoka nchini Afrika Kusini.
Katika mchezo huo Tp Mazembe waliibuka kidede kwa ushindi wa bao mbili kwa moja ushindi ambao hauwapi uhakika kushinda kombe hilo baada ya mchezo wa pili utakaopigwa nchini Afrika Kusini.
Tp Mazembe walipata bao la kwanza dakika ya 18 ya mchezo huo kupitia kwa Adama Troure kabla ya Sipho Mbuli kuwapatia wageni bao la kusawazisha, dakika ya 68 ya mchezo Daniel Nii Adjei aliipatia Mazembe bao la ushindi.
Dakika 10 za mwisho za mchezo huo zilikuwa chungu sana kwa Super Sports kwani Tp Mazembe walihamia katika goli lao huku muamuzi wa mchezo huo akiwanyima penati baada ya Solomon Asante kuchezewa rafu katika eneo la box.
Mchezo wa marudiano utapigwa siku nane zijazo ambapo Super Sport watahitaji ushindi wa bao moja tu ili kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo huku Mazembe wakihitaji sare tu ili kutawazwa kuwa mabingwa.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017