Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Tshishimbi Asubiriwa Dimba La Kati, Atakutana Na Hiki Chuma...






Kiungo mkabaji mwenye nguvu wa Singida United, Mudathir Yahaya amesema atahakikisha anapambana kumzuia kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshimbimbi katika mchezo kati yao leo kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.

Singida inayonolewa na Hans van Der Pluijm ipo nafasi ya sita katika Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 13 baada ya mechi nane, lakini Yanga inayofundishwa na George Lwandamina ni ya pili ikiwa na pointi 16.

Mchezo huo namba 66 wa ligi kuu unachezwa kwenye Uwanja wa Namfua ambao umekarabatiwa kwa kupandwa nyasi mpya sehemu ya kuchezea ambazo
zinachezewa kwa mara ya kwanza.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mudathir alisema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo kutokana na maandalizi waliyofanya.

“Mpango wangu ni kutibua mipango ya Tshishimbi ambaye anaonekana kuwa kero kwa timu pinzani, sikuwahi kumfuatilia kiungo huyo ila nasikia tu anasifiwa.

“Nimejipanga vizuri kwa kuhakikisha namdhibiti katika mchezo huu, sikuwahi kukaa kumfuatilia katika mechi alizocheza ili kuweza kujua uwezo na mbinu zake lakini nitamzuia.

“Timu nzima tunataka ushindi, tuna wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kupambana muda wote na kocha wetu ametuandaa vizuri,” alisema Mudathir anayecheza kwa mkopo Singida United akitokea Azam FC.

Katika mechi za kujiandaa na msimu huu wa ligi kuu, Yanga ilishinda   bao 3-2 dhidi ya Singida United.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017