Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeamua kuwaita waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi kuhusiana na tuhuma katika mkutano utakaofanyika leo.
Tuhuma wanazotaka kuzitolea ufafanuzi ni kuhusiana na kuelezwa kwamba kuna ufujaji wa fedha.
Tuhuma hizo zilikuwa zikisambazwa mtandaoni na mtu ambaye alipiga mahesabu ambayo sehemu kadhaa ualuonekana kuwa yamekosewa.
Hata hivyo, TFF inaonekana imeshindwa kuvumilia na Kaimu Katibu Mkuu, Wilfred Kidau ametangaza atazunguza na waandishi wa habari leo.
Lengo la Kidau kukutana na waandishi ni kutaka kutoa ufafanuzi ya madai hayo ambayo tayari wameyaita ni upotoshaji.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini