Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Ugomvi Wa Hadharani Wa Ramos Vs Ronaldo, Nani Mwamba Bernabeu?

Kumekuwepo na hali ya kutokubaliana na kutoa zinazotoa kutoelewana kwa wachezaji wawili wakubwa wa Real Madrid: Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos.
Huku matokeo ya uwanjani yakiwa ya kusuasua kwa ‘Los Merengues’ mwanzoni mwa msimu, wote wawili wamekuwa wakiulizwa nini kilichosababisha hali ya kutokuelewana, na imeripotiwa kwamba Nahodha wa Ureno ndio aliyeanza kutoa kauli zilizozalisha vita hiyo baridi waliyonayo.
Kufuatia matokeo ya kipigo dhidi ya Tottenham katika Champions League, Ronaldo alitoa kauli ambayo iliyoonyesha hakupendezwa na suala la kuuzwa kwa baadhi ya wachezaji muhimu wenye uzoefu katika timu hiyo, wachezaji kama James Rodriguez, Pepe, na Alvaro Morata.
Wakati maoni ya Ronaldo yakionekana ya msingi na yaliyopokewa na mashabiki na wachambuzi, Ramos alionekana wazi kukerwa na gazeti la El Chiringuito limeripoti nahodha huyo wa Madrid alikerwa sana na maneno ya Ronaldo.
Ramos ameeleza kwamba Madrid ilishinda mataji mawili mwanzoni mwa msimu bila uwepo wa hao wachezaji wanaolalamikiwa kuuzwa ambao CR7 anasema wamechangia kiwango chao kuporomoka, na baada ya hapo maelewano baina ya wawili hawa yakaendelea kupoteza muelekeo mpaka sasa.
Baada ya kipindi cha kiangazi kumetokea mabadiliko katika chumba cha kubadilishia nguo hasa baada ya wachezaji waliondoka kuwa ni marafiki wa Ronaldo. Wakiwemo wareno wenzie, Pepe na Fabio Coentrao na rafiki yake mwingine James Rodriguez.
Upande wa Ramos yeye amezidi kuwa na nguvu, hasa baada ya sera ya Zidane ya kuongeza vijana kikosi cha kwanza: wachezaji wengine kama Nacho, Dani Carvajal, Marco Asensio, Isco na Dani Ceballos – hawa wote ni wafuasi wa Ramos na hawawezi kusema chochote dhidi yake – kitu ambacho ni tofauti kwa Ronaldo.
Kingine kilichoongeza chumvi kwenye kidonda – ni maoni ya Ramos ya hivi karibuni – kwanza alipoanza kumzungumzia Neymar na suala la kuhamia Madrid, jambo ambalo kwa upande wa Ronaldo halikwenda vizuri, na kingine ni pale alipoulizwa kuhusu hatma ya uwepo wa Ronaldo Madrid.
“Cristiano anaondoka? Muulizeni mwenyewe, sifahamu lolote kuhusu yeye.”Alijibu Ramos baada ya sare ya Spain vs Russia – kauli ambayo inaelezww imezidi kuchangia ugomvi wake dhidi ya Ronaldo kuelekea mchezo muhimu wa wikiendi hii dhidi mahasimu wao Atletico Madrid.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017