Mkurugenzi wa Yamoto Band, Saidi Fella ‘Mkubwa Fella’ amedai kuwa hakuna msanii aliyekatazwa kuondoka ndani kundi hilo.
Aidha amedai kuwa wasanii wa bendi hiyo wanaruhusiwa kufanya project zao binafsi za muziki.
Fella ambaye ni mlezi wa wasanii 106, amesema kuwa kituo chake ni kama shule, yeyote ambae anajiona amekuwa anaweza kuondoka.
“Hakuna msanii ambaye amekatazwa kuondoka Yamoto Band hata Mkubwa na Wanawe ila ukiondoka bila kuaga haufiki sehemu yoyote,” alisema Fella.
Aliongeza, “Mimi nawasaidia kuwaonyesha njia wafike sehemu fulani, mtu akijiona amekuwa kwanini nimzuie?. Hakuna aliyefungwa kwa namna yoyote, sema ni vyema mtu kufuata taratibu hata za makuliano yetu ya mdomo,”
Pia Fella alidai hakuna msanii aliyekatazwa kuachia kazi zake binafsi.
“Aslay hivi karibuni ameachia kazi yake mpya na sisi tunamsupport kwa sababu kabla ya Yamoto Band, Aslay alikuwa msanii ila sisi tulimtumia yeye kuwainua wenzake na kweli tumefanikiwa leo hii vijana wanapata makate wao wa kila siku. Kwa hiyo hata wasanii wenzake wanaweza kufanya hivyo pia lakini kama wanamakubaliano yao binafsi siwezi kuyaingilia,” alisema Fella.
Bendi hiyo kwa sasa inafanya vizuri na wimbo ‘Basi’
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini