BARCELONA na Borussia Dortmund zimetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushindwa kupenya kwenye mechi za robo fainali ilizocheza dhidi ya Juventus na AS Monaco.
Barcelona iliyocheza na Juventus ilitupwa nje kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya sare ya 0-0 kwenye mechi ya jana Jumatano huko Nou Camp, huku Borussia Dortmund wao wakitupwa nje kwa jumla ya mabao 6-3 baada ya kuchapwa 3-1 usiku huo wa jana. Katika mechi za kwanza za hatua hiyo ya robo fainali, Barca ilichapwa 3-0 Turin, Italia wiki iliyopita wakati Dortmund wao walichapwa 3-2 kwao Ujerumani.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini