Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Dayna Akumbwa na Gonjwa la Kuweweseka

STAA wa Bongo Fleva, Mwanaisha Saidi ‘Dayna Nyange’ amefunguka kuwa siku za hivi karibuni amekumbwa na gonjwa la kuweweseka linalomkosesha raha.
Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Dayna alieleza kuwa kuweweseka huko kunatokana na msongo wa mawazo alionao kwani anawaza kazi mpya atakayoitoa baada ya Wimbo wa Komelo kuendelea kufanya vizuri kwani muziki kwa sasa una ushindani mkubwa mno.


  “Kiukweli ninavyowaza kuhusu ujio mpya mpaka najikuta naweweseka usiku wakati nikiwa nimelala, nikishtuka natuliza mawazo na kujipa moyo kuwa Mungu atanisaidia nitaandaa kazi nzuri ambayo itafika mbali zaidi ya hii niliyotoa sasa,” alisema Dayna.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017