Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Hivi Ndivyo Unavyojua Kama Una Upungufu Wa Maji Mwilini

Upungufu wa maji mwilini ni;
Pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji.

Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).

NINI HUSABABISHA?
Sababu zinazosabababisha mwili kukaukiwa maji huweza kuwa nyingi, lakini zinazojulikana zaidi ni pamoja na:

1. Kuacha kunywa maji
2.Kukaa kwenye joto kwa muda mrefu.
3.Kunywa kiwango kikubwa cha pombe
4.Ungonjwa wa kisukari ambao husababisha mtu kukojoa mara kwa mara.
5. Kutokwa na jasho jingi, kwa sababu ya ama kufanya kazi ngumu au mazoezi.

Hivyo inashauriwa mtu anayetokwa jasho jingi kunywa maji mara kwa mara wakati akiendelea na shughuli inayomtoa jasho.

Kama ukiugua au ukipatwa na homa kali, huweza kupungukiwa na maji mwilini
Kutapika na kuharisha nako huweza kupoteza maji mwilini. Hivyo itakeapo hali hiyo jitahidi kunywa maji mwilini.

Hizi ndizo dalili za kukaukiwa na maji mwilini kwa watoto wadogo;
Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.

Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:
  • Kukojoa mara chache sana
  • Mtoto kutokuwa mchangamfu
  • Macho.
  • Tumbo au mashavu kubonyea
  • Mdomo na ulimi kukauka.
  • Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.

Dadili za upungufu kwa wazee.

Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki.

Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.



Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017