Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Hizi Ndiyo Zinatajwa Kuwa Ndege Za Marais Zenye Gharama Zaidi Afrika


Afrika ni miongoni mwa bara lenye nchi nyingi maskini duniani lakini hii inaweza kukushangaza kwani kuna baadhi ya nchi zinatajwa kuwa na ndege za Rais zenye gharama kubwa ukilinganisha na ndege zinazomilikiwa na Marais wa nchi zilizoendelea kama Portugal.
Leo nimekutana na hii list ya Marais kumi kutoka Afrika wenye ndege za kisasa na zenye gharama zaidi barani Afrika hadi kufiki december 2016.
1:Morocco Boeing (747-400)

Hii ni ndege ya Mfalme wa Morocco inatajwa kuwa ndiyo ndege yenye gharama kuwahi kumilikiwa na kiongozi yoyote barani Afrika ambapo ina thamani ya zaidi ya dola milioni 450 ,ndege hii ina vyumba vitano va kulala,ukumbi wa mikutano na ukumbi wa kuangalia movie.


2: Zimbabwe (Boeing 767)
Licha ya Zimbabwe kuwa na hali mbaya ya kiuchumi lakini ndege ya Rais wa nchi hiyo ni ndege ya pili kwa kuwa na gharama barani Afrika ambapo ina thamani ya dola milioni 400 ina speed ya 858 km kwa lisaa na kuifanya kua moja ya ndege zenye kasi sana duniani.

3:Nigeria (Boeing 737)
Nigeria imeshika namba tatu kwa kuwa na ndege ya Rais yenye gharama barani Afrika ambapo ina zaidi ya thamani ya dola milioni 390.

4:Algeria (A340-500)
Ndege hii inayotumiwa na Rais wa Algeria ina engine zaidi ya nne,ina uwezo wa kusafiri angani kwa masaa 24 bila kutua ina vyumba maalum vya kupumzika na ukumbi wa mikutano.

5:Libya (A340)
Licha ya changamoto za kisiasa zilizopo Libya lakini nchi hii inatajwa kuwa na ndege ya Rais yenye gharama kubwa ambapo ina vyumba vya kulala,kumbi za mikutano ,jiko la kupikia na ukumbi wa sinema.

6:Egypt (Air Bus A340)
Egypt inatajwa kama nchi yenye ndege ya Rais ya gharama zaidi Afrika ambapo inavifaa maalum ambapo zitazuia ndege hii kusimama kwenye sehemu za hatari kama baharini au kwenye milima.

7:Ghana (Falcon 900 Ex Easy)
Ndege hii inatajwa kuwa na gharama ya dola milioni 37 na inauwezo wa kuwa angani bila kutua kwa masaa 13 .

8:Kenya (Fokker 70)
Hii ndiyo ndege maalum ya Rais wa Kenya ilinunuliwa mwaka 1995 inauwezo wa kubeba abiria 25 pia inauwezo wa kusafiri kwa 845 km kwa saa.

9:South Africa (Boeng 747)
Ndege hii ina uwezo wa kubeba watu 30 ina kumbi ya mikutano inayoweza kuchukua watu nane na ina vyumba vya kulala .


10:Angola (Embraer ERJ-135)

Ndege hii ya Rais wa Angola inashika namba kumi kwenye list ya ndege za Marais za kisasa na zenye gharama barani Afrika ambapo ina speed ya 834 km kwa saa moja .ndege hii ina vyumba vya kulala,sehemu za kulia chakula na kumbi za sinema.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017