Akiwa katika kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa na EATV, Harmorappa aliulizwa swali lililotumwa na shabiki aliyekuwa akifuatilia kipindi hicho ambalo liliuliza, “Wewe ni mwanaume wa aina gani?” na akijibu swali hilo alisema, “Mimi ni strong woman.”
Jibu hilo limewashangaza wengi kwa sababu Harmorappa ni mwanaume na hivyo wengi wameshindwa kuelewa kama alielewa swali liliuliza nini au alijibu kama utani.
Alipoulizwa kama anafahamu lugha ya Kiingereza, Harmorappa alisema anaielewa vizuri lakini tatizo ni kwenye kuongea.
Aidha, amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kujiendeleza kimasomo hasa kwenda chuo labda ajifunze zaidi lugha ya Kiingereza. Kuhusu suala la kujiunga WCB, alisema, “Siwezi kujiunga WCB hata kwa shilingi ngapi, Sizuzuki na hela, maana kama ni hela hata mimi mwenyewe ninazo.”
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini