Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kubeti Kwasababisha vijana kushindwa kutafuta fursa za kimaendeleo

Ongezeko la vijana kujiingiza katika michezo ya bahati nasibu hasa ya mchezo soka umeistua serikali kuona kupunguza nguvu kazi ya vijana katika kubuni mbinu mbadala za kujiongezea kipato na badala yake kufanya mchezo wa bahati nasibu kama sehemu ya ajira.

Akiongea mara baada ya kutembelea Maonesho ya Mifuko ya uwekezaji kiuchumi katika viwanja mashujaa mkoani Dodoma Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Dokta Khamis Kigwangala amesema mbali na sheria kuruhusu bahati nasibu izo vijana wanatakiwa kufanya mchezo huo kama burudani na kuungana na mikakati ya serikali ya awamu ya tano katika fulsa walizozitoa kwa wananchi kupitia mifuko ya kijamii na kuweza kujipatia mitaji ya kibiashara.

Kwa upande wa mifuko ya kijamii iliyoshiriki katika maonyesho hayo wameonyesha kujipanga katika kuakikisha wanawanufaisha watanzania katika kujiongezea kipato ikiwa ni utekerezaji wa mkakati wa serikali kufikia uchumi wa kati.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017